393. Dhambi Ikikulemea

1. Dhambi ikikulemea, 

   Kwa Bwana rehema;

   Hivi sasa tegemea 

   Neno la salama. 

        Tegemea, tegemea, 

        akwita sasa, Ni Mwokozi,

        ni Mwokozi, amini sasa.


2. Yesu amemwaga damu, 

   Ya nyingi baraka;

   Nawe sasa oga mumu

   Zioshwamo taka. 

        Tegemea ....


3. Ni njia Yeye hakika,

   Huongoza rahani;

   Usikawe kumshika,

   Uwe barakani 

       Tegemea ....


4. Karibu nawe wingie

   Mwetu safarini,

   Twende tukamwamkie,

    Milele Mbinguni. 

            Tegemea .... 

Popular posts from this blog

420. Ni Salama Mikononi Mwake

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

406. Mfurahini, Haleluya