Posts

Showing posts from May, 2025

339. Ee Ndugu, Twendeni Kazini

1. Yote namtolea Yesu,     Nampa moyo wote;    Nitampenda siku zote,    Namwandama kila saa.           Yote kwa Yesu,           yote kwa Yesu;           Yote kwako, Ee             Mwokozi,            Natoa sasa 2. Yote namtolea Yesu,    Nainamia pake;     Nimeacha na anasa,     Kwako Yesu nipokee.           Yote kwa Yesu… 3. Yote namtolea Yesu,     Nifanye niwe wako;     Nipe Roho wako, Bwana,     Anilinde daima            Yote kwa Yesu… 4. Yote namtolea Yesu,     Nami naona sasa     Furaha ya ukombozi;     Nasifu Jina lake            Yote kwa Yesu…

341. Haya, Umati wa Yesu

1. Haya, umati wa Yesu,     ulioungwa naye!     Haya, enendeni hima     katika vita kubwa!     Shetani tayari,     kupigana na sisi! 2. Tumfuate Yesu Kristo,     tumwamini Yeye tu.     Mwovu akituvizia     sisi hatuogopi.    Majeshi ya mbingu    ni pamoja na sisi! 3. Tukikesha na kuomba    Yesu anavyotaka,     tukishika Neno lake    na tukimtegemea     kwa nguvu hizi tu    tutaweza kushinda! 4. Sasa haya wenzi wangu,    tumfuate Yesu tu!     Siku za maisha yetu,    tuwe katika yeye.     Tuache dunia    kuingia mbinguni! 5. Pale Mungu atawapa     taji walioshinda,     wapate urithi wao     nyumbani mwa milele.     Hayani! Tuimbe,    tumsifu Bwana wetu! 

342. Ndugu Yangu Nani?

1. Ndugu yangu nani?    Umbu ni yupi?     Ni kila wa Yesu,     ni ndugu yangu. 2. Kikundi kidogo     chamjua Mchunga,    kimshuhudiacho     Mwokozi wetu. 3. Ni wana wa Mungu     wanaobezwa,    ndio washindaji     wangoja taji. 4. Ndio ndugu zangu,     maumbu yangu.    Nawaita hivi,    ni ndugu zangu.

343. Mwana wa Mungu Atoka

1.  Mwana wa Mungu atoka     kwenenda vitani,     bendera yake nyekundu;     utamfuata wee;      wataka kuungana      na maumivu yake?     Jitwishe msalaba wako,     nenda nyuma yake. 2.  Stefano aliuawa      kwa kumtegemea      ndiye aliyemtazama      ashindaye kufa.      Yeye kama Bwana wake     wakati wa kufa,      akawaombea wale      waliomwumiza. 3.  Na wale mitume tena      kumi na wawili,     Roho kawasaidia      kwenenda vitani.     Hawakuogopa kamwe      simba wala panga:      Roho utusaidie,      tukiwafuata. 4.  Jeshi kubwa lasimama      waume na wake      mbele ya kiti cha Bwana      na nguo nyeupe.     Wakajiponya mbinguni  ...

344. Watoto Wake Mungu

1. Watoto wake Mungu     imbeni safarini,    Mwokozi tutamsifu,     aliye mtakatifu. 2. Sote tu safarini,     tunakwenda mbinguni,    na tuone magumu,     jueni hayatakaa. 3. Watoto mwimbieni     inueni na macho!    Waliovumilia    wamekwisha ingia. 4. Ndugu tusiogope,     tutafika mbinguni,     Yesu akiwa nasi,     Shetani hatuwezi! 5. Bwana twakufuata,     ya chini twayaacha     U kiongozi wetu,     utatufikisha juu! 

345. Twalima na Kupanda

1.  Twalima na kupanda      mbegu shambani tu,      kukuza, na kustawisha      ni nguvu ya Mungu.      Umande hata mvua     na jua na mwezi,      anayetupa haya     ni Baba Mwenyezi.     Vitu vyote vyema      vyatoka kwake tu,      kwa hiyo tumsifuni,     tumshukuru Mungu! 2.  Vya mbali, vya karibu,      vyatoka kwa Mungu,      jua, mwezi na nyota,     kindege, bahari,     mimea ya mwituni,      vyakula vya shamba,     kwa mchana joto kali,      baridi usiku.           Vitu vyote … 3.  Ndiye aongozaye      mzunguko wa jua,      ni chimbuko la mwezi,     mwendo wa dunia.      Huwalisha wanyama,      wapate chakula,      watoto we...

346. Wajua Kuzihesabu Nyota

1.  Wajua kuzihesabu     nyota zilizoko juu?     Wajua kuyahesabu      nayo mawingu yote?      Mungu aliyahesabu      lisimpotee hata moja;     avijua kwa majina    2.  Wajua kuwahesabu      na ndege wa angani?      Wajua kuwahesabu      samaki wa majini?      viumbe vyake vyote.      Mungu huwapa kuwapo     huwaita kwa majina.      Kwa hiyo wanamchezea      na kumfurahia mno. 3.  Wajua kuwahesabu      watoto waamkao     asubuhi vitandani,      wacheze mchana kutwa,     Mungu huwatunza wote     kwa huruma zake kuu;      wewe nawe akupenda,     ndiye mpenda watoto.

347. Walio Watu Wake

1.  Walio watu wake,      awajua Bwana.      Wakubwa na wadogo      nchini popote.      Awahifadhi vyema,      hawataangamia.     /: Waishipo, wafapo      ni wake daima. :/   2.  Ajua kundi lake katika imani.      Wategemea yale wasiyoyaona.      Wazaliwa kwa Neno,      kwa Neno walelewa     /: nao kanuni yao      ni Neno la Mungu. :/ 3.  Ajua watu wake katika ushujaa     wa tumaini lao usio mashaka.      Ni miti istawiyo     katika mwanga wake,     /: mizizi yao hunywa      maji ya uzima. :/   4.  Ajua watu wake katika upendo      uzaao tunda jema      lipendezalo mno.      Hupenda ndugu zao      alivyotupenda,      /: na wao hubariki      ...

348. Kweli Yahuisha

1. Kweli yahuisha,     Maneno yenye uzima,    Muda unatosha,     wewe uweze kukoma.     Ni faida gani,    Wapata kwake Shetani?     Geukeni kwa Yesu rudini,    atakuponya dhambini.        Ee ndugu         muda wako unapita.         Ya kale yageuka na kupita.        Yale mapya          ndiyo sasa tunapata. 2. Wafikiri nini,  wewe usipofuata     mafunzo ya dini,     kama  ulivyoyapata?    Mchana u mwema,     usiku unageuka. Shika maonyo    vema daima, utaona ni baraka.          Ee ndugu … 3. Ni huzuni sana,    kwa watu wengi wa  Mungu,    kwa kutokazana     kuyafuata ya mbingu.    Wasikia mengi,    nao wayaacha tena.   ...

349. Nitamfuata Yesu

1. Nitamfuata Yesu,     mwenye huruma nyingi,     niishi kama yeye,     niishi kama yeye,    mwenye upendo mwingi. 2. Nitamfuata Yesu,    mwenye upendo mwingi,    apenda watu wote,     apenda watu wote,     ana huruma nyingi. 3. Nitamfuata Yesu,     anayetuombea,     niombe kama yeye,     niombe kama Yeye     Mwombezi wa dunia. 4. Nitamfuata Yesu,    mwenye upendo mwingi,     aita watu wote,    aita watu wote,    na wenye dhambi vivyo.

350. Maji Yako ya Akiba

1.  Maji yako ya akiba      yatakapopungua      uwakarimu wenzako     wasafiri njiani,     na hayo yatawatosha,     safari yenu yote.   2.  Kapu utakalotoa,      litajalizwa tena.      Vyakula vikipungua,      anga yafunguliwa      kilichotosha kwa mmoja,     kitatosha wawili. 3.  Sadaka iliyo hai,      Mungu huibariki.      Ghala za dunia hii,      nondo watamaliza.     Utabarikiwa sana      hazina ya mbinguni. 4.  Limbikiza juu mbinguni      kutu isikofika,      sadaka yako iliko      ndiko na moyo wako      utakapokaa nayo,      mbinguni juu milele. 5.  Roho ipendayo ndugu      ni maji ya uhai      ukimtazama Mwokozi,      u tajiri mbinguni...

351. Nataka Nimjue Yesu

1.  Nataka nimjue Yesu,     na nizidi kumfahamu,      nijue pendo lake, na      wokovu wake kamili.           Zaidi, zaidi,            nimfahamu Yesu,           nijue pendo lake, na           wokovu wake kamili. 2.  Nataka nimwone Yesu,      na nizidi kumsikia      anenapo Kitabuni,      kujidhihirisha kwangu.          Zaidi, zaidi … 3.  Nataka nifahamu, na       nizidi kupambanua      mapenzi yake, nifanye      yale yanayompendeza.             Zaidi, zaidi … 4.  Nataka nikae naye,     kwa mazungumzo zaidi,     nizidi kuwaonyesha      wengine wokovu wake.            Zaidi, zaidi … 

352. Ananipenda Kweli

1.  Ananipenda kweli      Neno lasema hivi      sisi watoto wake      hachoki kutulinda.      Yesu anipenda.      Yesu anipenda.      Yesu anipenda.     Mungu amesema. 2.  Kwa kupenda akafa      niokoke na kufa;      Atazisafi dhambi     kwake ataniweka.     Yesu ananipenda … 3.  Anipenda kabisa;      niuguapo sasa      anitunza mbinguni     niliyelala chini.     Yesu anipenda. … 4.  Kunipenda haachi,      tu sote hapa chini     baada ya mashaka      atanichukua juu.      Yesu anipenda.…

353. Twendeni Askari

1.  Twendeni askari,      watu wa Mungu;      Yesu yuko mbele,     tumwandame juu;      Ametangulia  Bwana vitani,     twende mbele      kwani ndiye amini.           Twendeni askari            watu wa Mungu:           Yesu yuko mbele,          tumwandame juu. 2.  Jeshi la Shetani, likisikia      Jina la Mwokozi litakimbia     kelele za shangwe zivume nchi;     Ndugu inueni zenu sauti:            Twendeni … 3.  Kweli kundi dogo,     watu wa Mungu,      sisi na mababa tu moja fungu,      hatutengwi nao, moja imani,      tumaini moja, na moja dini.            Twendeni... 4.  Haya mbele watu nasi njiani.     Inue...

354. Mteteeni Yesu

1.  Mteteeni Yesu, mlio askari;      Inueni beramu, mkae tayari;     Kwenda naye vitani,      sisi hatuchoki     hata washindwe pia     Yeye amiliki. 2.  Mteteeni Yesu, vita ni vikali;      Leo siku ya Bwana,      atashinda kweli;      Waume twende naye,     adui ni wengi     lakini kwake Bwana     tuna nguvu nyingi. 3.  Mteteeni Yesu, wenye  ushujaa;      Nguvu zenu za mwili      hazitawafaa;     Silaha ya Injili vaeni daima;      Kesheni mkiomba;      msirudi nyuma. 4.  Mteteeni Yesu, vita ni vikali,     wengi wamdharau,      hawamkubali,      ila atamiliki      tusitie shaka,      kuwa naye vitani     twashinda hakika.

355. Nikishika Njia Naona Mbali

1.  Nikishika njia     naona mbali mji ule kule      nitapafika.           Nisafiri sisahau ee            (safari, njoo fuate ee)            Usikie sauti yake ee            (Sikia sauti yake)              njoo sasa (ndugu)  2.  Njia yetu njema      katika Yesu twaona kwa mbali     mwanga wa mji.           Nisafiri …   3. Ingawa tufani    itusumbue twasogea pole    kuuendea.           Nisafiri …  4. Najua safari     sijui nyuma rangi za mji ule    zinanivuta.           Nisafiri …

356. Njia Ile Nyembamba

1.  Njia ile ni nyembamba      ya uzimani.     Heri anayefuata njia ile tu.           Ee nishike          (Bwanangu nishike Bwana)           nifike kwa Bwana.          (uzimani tu kwa Bwana)           Wewe ndiwe njia. 2.  Heri anayeamini asipoona.     Atapata kufahamu      yasiyoonwa.            Ee, nishike … 3.  Angalia ni mzima      aliyekufa,      Hivyo sote tu wazima      tukimwamini.             Ee, nishike … 4.  Ee, mwenzangu ukiomba     unikumbuke,      Niwe hai tangu sasa       na Yesu Kristo.              Ee, nishike …

357. Yesu Ndiye Njia

1.  K:  Yesu ndiye njia kweli,          tena Yeye ndiye uzima.     W:  Tena Yeye ndiye           mwanga,           nuru yake yaangaza.      K:  Bwana Yesu,     W:  Alikuja duniani          ili tuupate uzima. 2.  K:  Yesu ndiye mzabibu,          Mungu Baba ni mkulima      W:  Nasi tu matawi yake,         Kwa nguvu yake tutazaa      K:  Bwana Yesu,     W:  Atwalika watu wote,          tuzae matunda ya heri. 3.  K:  Yesu ndiye ufufuo,          ni uzima usiokwisha.      W:  Amwaminiye Yesu tu          ajapokufa ‘taishi.      K:  Sasa njooni,      W:  Sasa njooni kwake yeye;...

358. Anayemtumaini Mungu

1.  Anayemtumaini Mungu      siku zote kwa moyo mkuu,      ataona mastaajabu,      zikija shida na msiba.     Anayemngojea Mungu      amejenga juu ya mwamba. 2.  Tukisumbuka mchana kutwa     sababu ya shida zetu:     Tukilia usiku kucha      sababu ya msiba wetu      ni bure: Twazidisha tu      uchungu wa msiba wetu. 3.  Lakini tukivumilia      mizigo tuliyotwikwa,     na Baba yetu ajuaye      vizuri yanayotufaa,     tutapewa nguvu nyingi      za kuchukua huzuni. 4.  Ameiweka saa tayari      ya kupunguza mizigo.     Tukiwa wenye welekevu     katika kuvumilia,      mara atatuokoa     na kututendea mema. 5.  Katika shida usidhani:    “Mungu kaniacha sasa:     Lakini matajiri wote  ...

359. Nikiwa na Yesu

1. Nikiwa na Yesu, akiwa nami:    Mpaka nitakapokufa     sisahau pendo lake,     sioni huzuni    naona furaha na amani. 2. Nikiwa na Yesu naacha vyote,    namfuata Bwana wangu     siku zote kwa bidii; sitazifuata    njia pana za dunia hii. 3. Nikiwa na Yesu nayatumia    mambo yote ya dunia    Baba anavyopenda     nikimjua Yeye    siogopi mambo ya dunia. 4. Nilipo na Yesu ndipo pazuri.    Ninapata mema yote    kama mrithi wa Mungu;    ninapewa ndugu wapya ndio    Wakristo wenzangu.

360. Ninamwambia Mungu

1.  Ninamwambia Mungu      aliye Mwenye enzi      mambo yangu yote.      Asiposaidia     kwa tendo na baraka      siwezi kutenda kitu. 2.  Nikisumbuka sana,      usiku hata mchana,     ni bure kabisa.     Mungu  atamaliza      shughuli zangu zote      kama Yeye apendavyo. 3.  Namtumaini Bwana      anayenikingia     hatari na shida.      Nikimfuata Yeye      sitaona hasara,      sitapungukiwa kitu. 4.  Ana huruma nyingi     aondoa maovu,      afuta makosa.      Nijapokosa mengi,     hatanitupa mimi,     rehema yake ni kubwa. 5.  Nimempa Bwana huyu      moyo na mwili wangu,     hata kufa kwangu.     Akiniita kwake,     nitafuata hima.     Shauri...

361. Umngojee Bwana

1.  Umngojee Bwana,      moyo wangu,     umwambie yote,     ana huruma.     Acha hofu, jua likicha      giza linashindwa     na mchana mzuri.      Huzuni zako zikizidi,     Mungu wa rehema      akulinda. 2.  Umngojee Bwana,     moyo wangu,     umwambie yote,      ana huruma.      Zikivuma nguvu za      mwovu:     Bwana anaweza     kunyamazisha.      Wewe mwokozi,     nakungoja; niokoe nami,     Mungu wangu! 3.  Umngojee Bwana,      moyo wangu,      umwambie yote,     ana huruma.     Masumbuko yote yaisha      na kilio chetu kitageuzwa,     tutaipata raha bora.     Tumshukuru Bwana      Mungu wetu.

362. Umwekee Mwenyezi

1. Umwekee Mwenyezi     huzuni na shida    ulizo nazo kwako,    ana nguvu zote    Bwana atulizaye     bahari na pepo,     aweza kutuliza    hata moyo wako. 2. Bwana apenda sana    kubariki watu,     wanaokuja kwake     wakimtumaini.     Ukisumbuka sana    kwa uchungu mwingi,    hupati kitu kwake:    Ila ukimwomba. 3. Njia yako ikiwa     na giza na shida;    anazo njia Yeye     za kukuokoa.    Hakuna awezaye     kumzuia Mungu,     akitaka kufanya     mambo yake makuu. 4. Umtegemee Mungu     ukiona shida,    ana rehema nyingi    atakukumbuka,    saa yake ikifika.    Ungoje wakati    wa Bwana, utaona     jua la furaha. 5.  Naye akikawia  ...

363. Matendo Yangu Yoyote

Matendo yangu yoyote uyatengeneze Yesu!  Uniongoze popote,  nitakapokuwa leo, Amen. 

364. Mwanga Mkuu Ujao

1. Mwanga mkuu ujao,     utuangaze!    Tuyapambanue vema    maovu na mambo mema,       /: Utuangaze. :/ 2. Tulivyo duniani    hatuna wema,    macho yanaona woga,    mioyo inatetemeka,       /: Hatuna wema. :/ 3. Yesu tu ni Mwanga     wenye furaha.    Tupe kuitumaini    enzi ya utengemano,       /: Yenye furaha. :/ 4. Mwanga mkuu ujao,    utuangaze!     Roho zetu ziinuke,    na miguu ipate nguvu,        /: Utuangaze! :/ 

365. Sijui Njia Wewe Waijua

1.  Sijui njia, Wewe waijua,     kwa hiyo moyo unatulia.     Ni bure hata nikihangaika,      mchana kutwa hata na usiku. 2.  Wewe wajua njia hata mchana,     umekwisha tengeneza vyote.     Nakushukuru kwa upendo wako,     wanipenda kwa huruma yako. 3. Upendo ukivuma waujua,     wautuliza tu huchelewi.    Hunidanganyi na mimi nangoja,    Wewe wajua njia, yatosha!

366. Urudi Nyumbani

1. Urudi nyumbani, wewe mpotevu.    Kule ugenini hupati amani.          Ee mpotevu wee urudi           kwetu.          Njoo, njoo, njoo kwetu           njoo. 2. Urudi nyumbani, twakungojea.    Huzuni na toba ziongoe moyo.          Ee mpotevu wee … 3. Urudi nyumbani kutoka nchi    ya giza na hofu zikutaabishazo.         Ee mpotevu wee … 4. Urudi nyumbani    kwa Baba mwema.    Amekungojea    tangu siku nyingi.           Ee mpotevu wee … 

367. Mwokozi Yesu, Utangulie

1.  Mwokozi Yesu, utangulie      njia zote za maisha,      nasi tutakufuata,      utuongoze     mpaka mbinguni! 2.  Tunapoona shida zozote,      tuzivumilie vema,      tukumbuke; yatupasa      kwenda mbinguni     kwa shida nyingi. 3.  Mambo mabaya yakitujia,     tukiona ndugu zetu      wanashikwa na huzuni,      utukumbushe:     Raha i kwako! 4. Utuongoze njiani Yesu;    utulize mioyo yetu     hata siku za huzuni.     Tufungulie     mlango wa mbingu!

368. Vumilia Utaona Mwisho

1.  Vumilia utaona     mwisho kwamba umefika.     Kimebaki kitambo     kidogo tufike mbinguni.            /: Pokea (imani)              wokovu               ngao yako imani               nenda (mbele yake)               kwake Yesu Mwokozi:/ 2.  Kwa imani tutakwenda      mbele bila kulegea.     Wokovu ni wa thamani      kubwa kwa damu ya Yesu.           Pokea wokovu … 3.  Wasikia sauti yasema      amini Injili,      ukiwa katika giza kubwa     amini Injili.            Pokea wokovu …  4.  Imani kwa mambo     yaliyopo na yale yajayo,     mbele yetu ni njia ya kweli     Injili ya Yesu.   ...

369. Mungu, Niumbie Imani

1. Mungu, niumbie imani,     ipate kuzidi moyoni.     Imani (Imani, izidi moyoni).    Nipate kuona raha ya mbinguni.          (Nipate kuona            raha ya mbinguni)           /: Nipate ona yote            ya utajiri wako tu              uzidishe imani.:/ 2. Mungu, nijalie imani,    nipate shika Neno lako.            Imani (Imani, izidi) … 3. Imani huondoa shaka,     na matumaini huzidi.            Imani (Imani, izidi) …

370. Baada ya Kazi na Taabu Zote

1.  Baada ya kazi na taabu zote     nikiingia kwenye furaha,      kumwona Yesu,     kumwabudia,     kutakuwa furaha yangu kuu.           /: Kumwona tu ni furaha.:/            Nikiondolewa shida zote,            nikiona uso wa Bwanangu.   2.  Mwenye rehema anipendaye     akinipa kikao mbinguni,      nitamfurahia Mponya wangu     kwa kumwona tu uso kwa uso.           Kumwona tu …  3.  Pale mbinguni kwenye furaha     nitaonana na ndugu wengi.     Lakini kumwona Bwana Yesu     kutakuwa furaha kabisa.              Kumwona tu … 

371. Kwa Furaha ya Mbinguni

1. Kwa furaha ya mbinguni    umeitwa roho yangu, furahi!    Yesu akufungulia mlango wake,    ruka kwake kama tai.  2. Nitakaza mwendo sana    nifikie kundi la wateule,    waimbao na kusifu Bwana     Yesu pamoja na malaika.   3. Yesu Bwana wangu ng’oa     nanga ya mashua yangu upesi,    niingie bandarini mwa amani    na kuona raha kuu. 4. Yesu wangu sitakoma kukusifu,    kwani umeniponya.    Roho yangu yatamani kukuona;    Bwana njoo, nichukue! 5. Unaweza kwa haraka     kugeuza woga uwe furaha.    Unatupitisha kufa kama ndoto:    mara tutafufuka. 6. Umevumilia shida hata kufa    tusishindwe na kifo.     Sasa kufa kumeshindwa,    nao mwili wangu utafufuka.

372. Tegemea Mpaka Kufa

1. Tegemea mpaka kufa,     utapata wokovu.    Bwana Yesu ni Mwokozi    Yeye anakupenda.    Uje kwake ’sikawie,    Yeye akuokoa.    Njoo upesi! Njoo upesi!     Fika kwa Bwana Yesu. 2. Acha mambo ya  dunia    yakuhangaishayo.    Iko mali ya uzima     unaitiwa hiyo.    Mali hiyo ni uzima    utapewa na Bwana.     Njoo upesi! … 3. Wakatae, waepuke     wanaokudanganya;    ni wajinga, wakuponza,     wakupoteza wewe.    Ila wewe ukatae     kuondoka kwa Yesu.    Njoo upesi! … 4. Ukijua jambo hilo usipolifuata    kosa hilo kubwa sana,     wapasiwa hukumu.    Vumilia, jizuie utapata uzima.         Njoo upesi! … 5. Bwana Yesu amekwisha     kukutengenezea     kitu chema kwake Mungu,  ...

373. Nyumbani, Nyumbani

1.  K:  /: Nyumbani,      W:  Nyumbani            ni  Yerusalemu:/      K:  Ndipo mahali,      W:  Ndipo mahali niendapo.     K:  Jamani,     W:  Jamani ninakwenda,         /: Natamani makao ya          Yerusalemu. :/ 2.  K:  /: Kesheni,     W:  Kesheni siku itakuja. :/      K:  Tutaonana,     W:  Tutaonana na Bwana     K:  Vizuri,     W:  Vizuri kumtazama,          /: Tumtazame Mwokozi           mwenye utukufu. :/ 3.  K:  /: Kwa Yesu,      W:  Kwa Yesu   nimetumaini. :/      K:  Twende zetu, wee,      W:  Twende zetu,          wee mwenzangu.      K:...

374. Nchi Nzuri Yametameta

1.  Nchi nzuri yametameta,     huonekana kule mbali,      naye Yesu hutuongoza.      Tufike na sisi huko.         /:Si mbali, karibu,           tutaimba na sisi huko!:/ 2.  Kule tutawaona wengi     wapendwao na Yesu Bwana,     Tutashirikiana nao       itakuwa furaha kubwa.           Si mbali … 3. Tutamwona na Bwana wetu,    Yesu Kristo Mwokozi wetu,    Tutashangilia daima,     tuna hamu ya kwenda kwetu.            Si mbali …

375. Ni Wako Mungu, U Furaha Yangu

1.  Ni wako Mungu,      u furaha yangu,     ni neema kumjua     Mwokozi wangu.           Haleluya atukuzwe,            Haleluya amen;            Haleluya atukuzwe,            ukarudi Yesu! 2.  Mwana wa Mungu      ndiye fungu langu,     moyo wanitulia      kwa Yesu wangu.           Haleluya, atukuzwe, ... 3.  Nikishapatwa      na mapenzi haya,      nimepata uzima      na mbingu pia.            Haleluya, atukuzwe, … 4.  Nchi niendayo,      nenda mbio mbio      ina karamu kweli,     ya humu siyo,            Haleluya, atukuzwe, … 5.  Twaionja humu      tulimo nchini,     mpaka tufike...

376. Yasikilizeni Haya

1. Yasikilizeni haya    watu wa dunia wote:     Mwokozi mara ya pili     yuaja atuamue. 2. Haji tena kama kwanza    na hali ya umaskini.    Ila kwa kuzionyesha     nguvu zake duniani.   3. Hao wampendao sasa    weupe hata weusi.     Watamwona akishuka     na enzi kuu mawinguni. 4. Siku hiyo ya hukumu     mimi nitakuwa wapi,    watakapoitwa wote,    walalao kaburini? 5. Yesu Bwana nakuomba:    Sasa unihurumie,    kuitenda kazi yako,    hata urudipo hapa!  

377. Atashuka na Mawingu

1. Atashuka na mawingu     aliyewambwa mtini,    na watakatifu wengi     watamtukuza sana.        /: Haleluya, Haleluya,           Haleluya, :/           Yesu anatujia!  2. Kila jicho litamwona     katika enzi yake,    nao waliombeza     wataogopa wote,         /: Watalia, watalia,          watalia, :/           wakimwona Mwokozi. 3. Na alama za vidonda    hata sasa anazo,    nao watumishi wake     wakombolewa nazo,         /: alipata, alipata,         alipata, :/         makovu kweli kwao. 4. Wapaangukia wote      penye kiti cha enzi.    Vaa Mwokozi nguvu zote     Njoo sasa kumiliki!  ...

378. Pana Jito, Lina Maji Mazuri

1.  Pana jito, lina maji mazuri,     yaenda ulimwenguni.      Lametameta nalo linang’aa.      Walijua jito hilo?     Ninakuita nawe njoo!      Utafute jito hilo!      Maji yake yapoza moyo.      Nawe yateke unywe. 2. Wanywao maji haya wafurahi,    waimba kwa shangwe kubwa.     Makosa na shida yanaondoshwa,    wote waoshwa na Bwana.         Ninakuita nawe njoo … 3. Jito hilo latoa maji mengi,     matamu yapendezayo.     Yaponya wagonjwa,     yatia nguvu, uchafu watakasika.           Ninakuita nawe njoo… 4. Maji ya jito hilo ni uzima     unaotoka kwa Yesu.     Damu yake yenye kiasi kikuu     imemwagwa tusafike.           Ninakuita nawe njoo … 

379. Kule Mbinguni Nataka Kwenda

1. K:  Kule mbinguni nataka         kwenda, nitawezaje          kufika huko?    W:  Yesu ni njia tena Uzima,         Tukimwamini          ndipo twafika. 2. K:  Kule mbinguni         ni kwema sana,        Ndiko maskani          kwa Mungu Baba.     W:  Yesu ni njia, tena Uzima,         Tukimwamini            ndipo twafika. 3. K:  Mungu Mwenyezi         Mwenye uzima,         Ndiye mleta wetu uzima    W:  Yesu ni njia, tena Uzima,         tukimwamini            Baba twamwona. 4. K:  Mungu ni pendo,         apenda watu        ...

380. Mungu Tangu Mwanzo

1.  Mungu tangu mwanzo     ameandaa     wokovu kwa wote, pia na njia     kwa wanaoishi, kutopotea.     Waje kwake tena, awaridhia.     Kayatimiza yote,      ya kuokoa wote      nitajiteteaje? Sina udhuru,      sina udhuru,      sina mbele za Mungu 2. Adamu wa kale, hakutubia,    uasi kwa Mungu, ajitetea.     Hoja yake kubwa, kasingizia,    Mungu kaamua, kuhurumia.    Kayatimiza yote … 3. Maarifa mengi yameingia,    na watu wazidi kwa kukosea     wavunja adili na uraia,    Mungu sasa aja na mausia.     Kayatimiza yote … 4.  Maajabu mengi ya kuvutia,     na wajumbe tele atutumia,     alimtuma Yesu kutukomboa,     akafanya mengi, na kutufia.     Kayatimiza yote ... 5.  Sisi tukiishi atungojea,      atuvumilia, geuza nia...

381. Kuna Nchi Nzuri Sana

1.  Kuna nchi nzuri sana      na utukufu mkubwa mno,      Neno hilo lapendeza,     siku nitakapofika!  2.  Njia zake za dhahabu      na lulu za thamani kuu,     kuna na mengi ajabu,      siku nitakapofika! 3.  Watu wake ni wazuri,     kwao hakuna wadhambi,     huishi kwa furaha tu,     siku nitakapofika!   4.  Sauti zao ni nzuri,       huku hazipatikani,      ni sauti za ajabu,      siku nitakapofika! 5.  Ndio watoto wa Mungu      wenye upendo wa kweli,     mavazi yao meupe,      siku nitakapofika! 6.  Bwana wetu tuandae,      tuweze kufika huko,     ili tushiriki nao,     pawe ni makao yetu!

382. Kuna Nchi Nzuri Isiyo na Dhambi

1. Kuna nchi nzuri isiyo na dhambi,         /: Wazee wema,            wazee wema           waimba haleluya. :/ 2. Kuna nchi nzuri haina majonzi,         /: Wazazi wema          wazazi wema           waimba haleluya. :/ 3. Kuna nchi nzuri isiyo na taabu,          /: Watoto wema,            watoto wema            waimba haleluya. :/  4. Kuna nchi nzuri isiyo na shida,          /: Vijana wema,              vijana wema             waimba haleluya. :/ 5. Kuna nchi nzuri haina majuto,           /: Watoto wema,             watoto wema             waimb...

383. Ulimwengu Hayani

1. Ulimwengu hayani,    tumsifu Mungu wetu.    Alimtoa Mwanawe,    Yesu Kristo Mkombozi!    Haya, twendeni kwa Yesu! 2. Kwani sisi hatuna     hata mtu msemi,     awezaye kufanya haki     mbele ya Mungu:    Haya twendeni kwa Yesu! 3. Yesu ni kiongozi    wa ulimwengu wote,     ajuaye njia tu,    iendayo kwa Mungu:    Haya, twendeni kwa Yesu.

384. Mungu Akitupa Kipaji

1.  Mungu akitupa kipaji      kilicho kizuri zaidi     atusafirisha duniani,     tuone mazuri yake. 2.  Mwoga hataki kwenda mbali,     hupenda kuwa kwao tu,     afanana na vifaranga      wasiotoka kwa mama. 3.  Mito yaporomoka sana     na ndege wanaimba juu,     tunashirikiana nao     kwa furaha za mioyo. 4.  Mungu wetu na asifiwe!     Hulisha ndege, wanyama,     dunia na mbingu ni zake,     yee hatatusahau nasi. 

385. Nitayainua Macho Yangu

Nitayainua macho yangu  niitazame milima.  Msaada wangu utatoka wapi?  Msaada wangu u katika Bwana.  Aliyezifanya mbingu na nchi. Asiuache mguu wako usogezwe.  Asisinzie akulindaye.  Naam, naam, naam.  Hatasinzia wala hatalala usingizi.  Yeye aliye mlinzi wa Israeli.  Bwana ndiye mlinzi wako.  Bwana ni uvuli mkono wako wa kuume. Jua halitakupiga mchana wala mwezi wakati wa usiku.  Bwana atakulinda  na mabaya yote.  Bwana atakulinda  na mabaya yote.  Atakulinda nafsi yako.  Bwana atakulinda,  Utokapo na uingiapo.  Tangu sasa na hata milele   

386. Aitwa na Simanzi

1.  Aitwa wa simanzi     Mwana wa mwenye enzi,      Mwenye mengi mapenzi,      Haleluya Bwana Yesu. 2.  Alikuwa dhikini,     Bwana Mwokozi wangu      Akatoka mbinguni,      Haleluya Bwana Yesu. 3. Tu wenye dhambi sana,    Kwake dhambi hakuna,    Na Mungu twapatana    Haleluya Bwana Yesu  4. Akapata uchungu     Akalia dhikini    Sasa yuko mbinguni    Haleluya Bwana Yesu  5. Punde atarejea     Yesu kutunyakua     Ndipo  tutamwimbia     Haleluya Bwana Yesu

387. Anza Yote na Bwana

1. Anza yote na Bwana;     Umwamini kama mtoto     Anavyomwamini baba;     Nawe ufanye hivyo.           :/:Anza yote na             Bwana.:/:   2. Anza yote na Bwana;     Enyi wateule wake     Msipoteze lengo lake,     Nenda njia ya Bwana.            :/:Anza yote… 3. Anza yote na Bwana;     Uwe jasiri kwa Bwana,    akupa msaada wake,    Ufanye kazi yake           :/: Anza yote…   4. Anza yote na Bwana;     Atatuma roho wake      awe mfariji wako     Kwenye maisha yako           :/:Anza yote ....

388. Asante Sana Yesu

1. /:Asante sana Yesu,     asante sana Yesu.     Asante sana Yesu moyoni:/  2. /:Dhambi zatakasika,     Dhambi zatakasika.     Dhambi zatakasika moyoni:/ 3. /:Siishi bila Yesu    Siishi bila Yesu    Siishi bila Yesu moyoni:/ 4. /:Magonjwa yanapona    Magonjwa yanapona     Magonjwa yanapona moyoni:/  5. /:Amani tunapata    Amani tunapata     Amani tunapata moyoni:/  

389. Ashukuriwe Mwenyezi

1.  Ashukuriwe mwenyezi.     Ametujalia mengi.     Ni ukarimu wake mkuu      kwetu milele.           Tuwe naye pote pote             duniani,            Tuwe naye pote,            (Tumsifu pote)            Safari hii yetu duniani.            Tukiwa naye  mwenyezi           hatuna woga. 2.  Hata tukiwa gizani,     mwanga wake watutosha.      kwa neno lake tapita      vipingamizi.             Tuwe naye pote pote....  3.  Nazo hatari za njia,     zikitujia, ee Bwana,      msaada wetu ni wewe,      utawalaye.             Tuwe naye pote pote....  4. Tunatazama mbinguni,  ...

390. Bwana Asema Nimtume Nani

1. Bwana asema     Nimtume nani    /:Na ni nani      atakayekwenda     badala yetu:/         Nitume mimi Bwana         X 4 X 2 2. Midomo yangu    Michafu sana    /:Uichome kwa kaa     la moto unitakase:/           Nitume mimi.... 3. Ninaogopa    Umri  mdogo    /:Kuhubiri Neno lako    Bwana huko niendako:/             Nitume mimi.... 4. Waniambia:    “Usiogope,     /:utapata ujasiri       mwingi: kutoka kwangu.”:/              Nitume mimi.... 

391. Bwana Mungu, Nashangaa

1. Bwana Mungu,    nashangaa  kabisa    nikitazama kama vilivyo;     nyota, ngurumo,     vitu vingi vyote     viumbwavyo     kwa uwezo wako          /: Roho yangu na ikuimbie          Jinsi wewe ulivyo Mkuu.:/ 2. Nikitembea pote duniani,     ndege huimba, nawasikia;    milima hupendeza macho sana,    upepo nao nafurahia         /:Roho yangu… 3. Nikikumbuka kama     Wewe Mungu     ulivyompeleka mwanao,    afe, azichukue dhambi zetu    kuyatambua ni vigumu mno.           /: Roho yangu..... 4. Yesu Mwokozi utakaporudi     kunichukua kwenda    mbinguni, nitashukuru     na kwimba milele     Wote wajue jinsi ulivyo.          /:Roho yangu …

392. Bwana Yesu Aliteswa

1.  K:  /:Bwana Yesu aliteswa,     W:  Bwana,  kweli Bwana           walimtenga Bwana:/           /:Wanafunzi walimtesa            Bwana, wakamwacha              peke yake, Bwana.:/      K:  /:Kweli Yesu aliteswa,:/      W:   /:Bwana, walimtesa               msalabani, Bwana.:/ 2.  K:  /:Na askari wakambeza,      W:  Bwana, wakamwudhi            kwa Pilato, Bwana:/         /:Nguo zake wakamvua,          Bwana, wakamvika vazi           safi, Bwana.:/     K:  /:Kweli Yesu aliteswa../ 3.  K:  /:Hata taji ya miiba,      W:  Bwana, wakamvika         ...

393. Dhambi Ikikulemea

1. Dhambi ikikulemea,     Kwa Bwana rehema;    Hivi sasa tegemea     Neno la salama.          Tegemea, tegemea,          akwita sasa, Ni Mwokozi,         ni Mwokozi, amini sasa. 2. Yesu amemwaga damu,     Ya nyingi baraka;    Nawe sasa oga mumu    Zioshwamo taka.          Tegemea .... 3. Ni njia Yeye hakika,    Huongoza rahani;    Usikawe kumshika,    Uwe barakani         Tegemea .... 4. Karibu nawe wingie    Mwetu safarini,    Twende tukamwamkie,     Milele Mbinguni.              Tegemea .... 

394. Deni ya Dhambi Ilimalizikia

1. Deni yangu ya dhambi,     Yesu amelipa.    Kwake Msalabani     Nilipewa Uzima         Deni ya dhambi,         Msalabani          Ilimalizikia         Ni huru kabisa. 2. Bwana Yesu asema,   “Mwanangu dhaifu,    Uwezo na ushindi    Hupatikana kwangu.”          Deni ya dhambi,... 3. Bwana, kweli naona,     Nguvu zako pekee     Huondoa ukoma,     Niwe kipya kiumbe.          Deni ya dhambi,... 4. Sina wema moyoni,     Nidai neema,     Nakubali kabisa,    Kwa damu kusafiwa.        Deni ya dhambi,... 5. Hata huko Mbinguni,    Miguuni pake,    “Yesu alinifia,”      Nitaimba milele.            Deni ya dhambi,...

395. Ee Yesu, Unapenda Wote

1.  K:  /:Ee Yesu, unapenda wote,     W:  Na mimi wanipenda.:/           Nikutumikie maisha yote,          mwokozi wangu, wee           milele nipate kuishi kwako,          mwokozi wangu wee.   2.  K:  /:Ee Yesu, unaponya           wengi,     W:  Na mimi waniponya.:/           Nikutumikie maisha ...  3.  K:  /:Ee Yesu, ndiwe          Mchunga mwema,      W:  Na mimi wanichunga.:/           Nikutumikie maisha ... 4.  K:  /:Ee Yesu, ulisulibishwa,     W:  Nipate kuokoka.:/          Nikutumikie maisha ... 5.  K:  /:Ee Yesu, ulifufuliwa,      W:  Na mauti ulishinda.:/          Ni...

396. Furahini Wote

1.  K:  Furahini wote     W:  Furahini wote     K:  Mwokozi yu hai     W:  Mwokozi yu hai          /:Amefufuka, amefufuka,            Mwokozi wetu Yesu:/  2.  K:  Msifuni wote     W:  Msifuni wote     K:  Ameshinda kifo     W:  Ameshinda kifo          /:Amefufuka,....  3. K:  Himidini wote    W:  Himidini wote    K:  Ameshinda yote    W:  Ameshinda yote          /:Amefufuka,....  4. K:  Shukuruni wote     W:  Shukuruni wote      K:  Ushindi ni wake     W:  Ushindi ni wake         /:Amefufuka,....   5. K:  Msihofu wote    W:  Msihofu wote     K:  Tunaye Mwokozi ...

397. Haleluya Tumwimbieni

1. K:  Haleluya tumwimbieni     W:  Bwana, Haleluya          tumwimbieni Bwana    K:  Mtukuze    W:  -kuze Mungu,     K:  Mshukuru     W:  -kuru ndiye      K:  Mwokozi.     W:  -kozi wetu. 2. K:  Katika Neno twaambiwa    W:  Kweli. Katika Neno          twaambiwa kweli     K:  Mtukuze .... 3. K:  Hakika, pendo lake Mungu    W:  Kubwa. Hakika, pendo           lake Mungu kubwa.    K:  Mtukuze .... 4. K:  Mwokozi Yesu katujia    W:  Sisi. Mwokozi Yesu         katujia sisi.     K:  Mtukuze ... 5. K:  Wokovu alituletea      W:  Wote. Wokovu          alituletea wote. ...

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

1. Hapana rafiki kama Yesu,    Yu pekee, Yu pekee;    Hapana mpozi kama Yesu     Yu pekee, Yu pekee.            Yesu ajua shida zetu,            Aweza kutuongoza;            Hapana rafiki kama Yesu,            Yu pekee Yu pekee. 2. Yeye anaye sifa, ni Yesu    Yu pekee, Yu pekee;     Ndiye aliye Mnyenyekevu    Yu pekee, Yu pekee;             Yesu ajua...... 3. Yesu pamoja nasi daima,    Yu pekee, Yu pekee;     Kwa usiku aleta salama,    Yu pekee, Yu pekee;            Yesu ajua...... 4. Kulinda Yesu Yu Mwaminifu,    Yu pekee, Yu pekee;    Atawakubali wahalifu,     Yu pekee, Yu pekee;             Yesu ajua...... 5. Alipel...

399. Hata Ndimi Elfu

1.  Hata ndimi elfu elfu,     /:Hazitoshi kweli:/      Bwana Yesu kumsifu,      Kwa zake fadhili. X3 2.  Yesu jina liwezalo     /:Kufukuza hofu:/        Lanifurahisha hilo,     Lanipa wokovu. X3 3.  Jina hilo ni uzima;     /:Ni afya; amani:/       Laleta habari njema;      Twalipiwa deni. X3 4.  Yesu huvunja mapingu     /:Ya dhambi moyoni:/       Msamaha, tena nguvu,       Twapata Rohoni. X3 5.  Kwa sauti yake vile      /:Wafu hufufuka:/        Wakafurahi milele,       Pasipo mashaka. X3 6.  Ewe Yesu wangu Bwana     /:Uwezo nipewe,:/      Kuhubiri kote sana,      Wote wakujue. X3  

400. Imezuka Siku ya Neema

1. Imezuka siku ya neema,     mfano wa pambazuko;     yenye mwanga toka     Mungu juu furaha ikamilishwe.    Mungu ndiye nuru gizani    akae mioyoni mwetu 2. Imezuka siku ya neema,    Mwokozi katutokea;     ulimwengu wote upewe     furaha pasipo mwisho.     Yesu atupenda kabisa,    fedheha amefukuza. 3. Alibeba dhambi, si zake,    alipotundikwa mtini.    Kifo hakikumweza Kristo.     Mwamba akauondoa,    Ili sisi na jeshi la juu     tumwimbie siku zote. 4. Baada ya siku hamsini     akatumwagia roho,    ili tusibaki gizani,    na kupotelea mbali.     Moto wake watutakasa,     na kutuponyesha kweli.  5. Safari ya mwisho yaiva,     tuitwapo naye Kristo.     Sote tutaimba kwa shangwe    pamoja na ...

401. Jina la Yesu, Salamu!

1.  Jina la Yesu, salamu!     Lisujudieni,     ninyi mbinguni, hukumu     na enzi mpeni. 2.  Enzi na apewe kwetu,     watetea dini;     mkuzeni Bwana Mungu wenu,     na enzi mpeni. 3.  Enyi mbegu ya rehema,      nanyi msifuni;     mmeponywa kwa neema,     na enzi mpeni. 4.  Wenye dhambi kumbukeni     Ya Msalabani,     Kwa furaha msifuni,     Na enzi mpeni 5.  Kila mtu duniani     Msujudieni,     Kote kote msifuni,     Na enzi mpeni 6.  Sisi na wao pamoja      Tu mumo sifani,      Milele sifa ni moja,      Ni enzi mpeni. 

402. Kale Nilitembea

1.  Kale nilitembea,     nikilemewa dhambi      nilikosa msaada,      kuniponya mateso.            Usifiwe Msalaba!            Lisifiwe kaburi!            Linalozidi yote,            Asifiwe Mwokozi! 2.  Hata nilipofika,      mahali pa Msalaba,      palinifaa sana,     sitasahau kamwe.             Usifiwe... 3.  Hicho ndicho chanzo,     cha kufurahi kwangu.     hapo ndipo mzigo,     uliponituliwa.              Usifiwe... 4.  Panapo Msalaba,      kinatolewa cheti,     cha kuingia Mbinguni,     kisicho cha kanisa.            Usifiwe... 5.  Yule bwana mjinga,      likwenda bila cheti,   ...

403. Katika Neema ya Yesu

1. Katika neema ya Yesu     nimeokolewa,     nilipotea dhambini,    kipofu rohoni. 2. Bali neema ya Yesu     yanitosha sana     ilinifumbua macho     ikanifungua. 3. Nilikuwa mwenye hofu    nilifungwa nazo,    nimefunguliwa sasa    kwa neema ya Yesu. 4. Nitamsifu Bwana wangu    maishani mwote,     kwani nina ushirika    Msalabani mwake. 5. Tutakapofika wote     mbinguni kwa Mungu,     tutashukuru neema    ya Yesu milele.

404. Kituo changu hapa katika Yesu.

1. Kituo changu hapa katika Yesu.     Sipiti, sipiti, hapa napumzika.           Ee Yesu Bwanangu.           Sitapita (mwenzangu)            ee sitapita (mwenzangu)           ee japo nikiwa shidani           (sipiti, mwenzangu).           Napumzika hapa kwa Yesu. 2. Mizigo yangu hapa katika Yesu,    msalaba, msalaba,    kivuli changu chema.           Ee Yesu... 3. Amani yangu hapa katika Yesu.    amani, amani, ya roho nimepata.            Ee Yesu... 

405. Mbele Nina Endelea

1.  Mbele ninaendelea,      ninazidi kutembea;      Maombi uyasikie,     Ee Bwana, unipandishe.            Ee, Bwana, uniinue,              kwa imani nisimame;             nipande milima yote,              Ee Bwana, unipandishe. 2. Sina tamani nikae,    mahali pa shaka, kamwe;     Hapo wengi wanakaa,    kuendelea naomba.            Ee, Bwana.... 3.  Nisifungwe na dunia,     asumbuapo Shetani;     natazamia mbinguni,     nitafika na imani.            Ee, Bwana.... 4.  Nataka nipandishwe juu,     zaidi yale mawingu;      nitaomba nifikishwe,     Ee, Bwana, unipandishe.          Ee, Bwana.... 

406. Mfurahini, Haleluya

1.  K:  Mfurahini, Haleluya,         Mkombozi amefufuka.          Amefufuka, Haleluya.          Msifuni sasa yu hai.      W:  /:Tumwimbie sote           Yesu ametoka kaburini.          Kashinda kifo, Haleluya,         Haleluya, Yesu yu hai.:/ 2.  K:  Amefufuka Mkombozi,         Haleluya, tushangilie.         Nguvu za mwovu           ameshinda          Ametuondoa kufani.       W:  /: Tumwimbie sote... 3.  K:  Malaika aliwaambia          wanawake, “Msiogope.          Sasa kaburi lipo tupu,          kwani Yesu amefufuka.”     W:  /:Tumwimbie sote... 4.  K:  “Amebatilisha Shetani....

407. Mibaraka Tupe Mibaraka

1. Mibaraka tupe mibaraka    Mibaraka tupe mibaraka     Toka kwako.    Mungu Baba Mungu twakuomba,        /:Tunakuomba libariki    Kanisa lako Baba:/     Liwe na umoja na upendo.  2. Wachungaji na Maaskofu,    Wachungaji na Maaskofu    wabariki,    Na Wainjilisti wabariki.     /:Uwape moyo wa hekima     katika kazi yako:/    Wajenge Kanisa kwa upendo 3. Mungu Baba Mungu twakuomba    Mungu Baba Mungu twakuomba    tubariki;    Hata na Wakristo wabariki    /:utupe moyo wa hekima katika    kazi yako:/     Tujenge Kanisa kwa upendo. 4. Waamini pote duniani Waamini    pote duniani wabariki;    Hata na Wazee wa Kanisa    /:uwape moyo wa hekima     katika kazi yako:/    Wajenge Kanisa kwa upendo.

408. Mimi ni Mzabibu

W: Mimi ni mzabibu,     Mimi ni mzabibu,     nanyi ni matawi Yangu,     nanyi ni matawi Yangu.     1. K:  Kaeni ndani yangu,         nami ndani yenu,         kwani mu matawi,         nami kweli ni mzabibu.     W:  Mimi ni mzabibu,... 2. K:  Nje yangu mimi,         hamwezi kuzaa,         kwani mu matawi,...   3. K:  Tawi lizaalo, lizidi kuzaa,        kwani mu matawi, .... 4. K:  Furaha yangu,          iwe ndani yenu,         kwani mu matawi,... 5. K:  Ombeni lo lote         nanyi mtapewa,         kwani mu matawi,... 6. K:  Amri yangu ndiyo,         mpate kupendana,        kwani mu mata...

409. Mjini Kwake Nazareti

1.  Mjini kwake Nazaret     kasema Yesu wazi,     yakuwa kwake unabii     wa kale umetimia.         /:Kusaidia maskini,             vipofu nao waone,           wafungwa wawe huru tu,            wasetwa wawe wazima.:/ 2.  Wazee walishangazwa tu      na mahubiri yake.      Huenda huyu ni nabii     na hata Kristo Masihi.        /:Kusaidia maskini,... 3.  Maisha’ke shuhuda kuu,      maneno yake kweli.      mpaka kufa kawa mtii,     kawambwa msalabani.           /:Kusaidia maskini,... 4.  Wenzangu, muwe mashujaa,     kumshuhudia pote.     Mwokozi Yesu yu pekee,     na hivyo akatujia.            /:Kusaidia maskini,... 

410. Mtolee Bwana

1. Mtolee Bwana  katika maisha     matunda ya pendo,    yale yapasayo,     tumtolee Bwana.    Tushukuru yale yatokayo kwake     kwa neema kubwa.        /:Tutoe sadaka          tumshukuru Bwana:/ 2. Atupa maisha, akili, uweza;    atupa nyakati za kufanya kazi;     na hiyo ni neema.     Na mali nyingine zinatoka    kwake kutufurahisha.         /:Tusifu na nini         kwa vipaji vingi?:/ 3. Sisi twazaliwa, katika ukiwa.    Mungu peke yake,     ndiye atoaye;     kwetu kwa huruma.     Tu wakili wake;     hayo tuyatunze na tusitawanye.        /:Kutoa tutoe;           talanta ni zake.:/ 4. Fundisho ni kubwa:    Mjane katoa mali yake yote,   ...

411. Mungu Mtatu Ndiye Muumba

1.  K:  Mungu Mtatu          ndiye Muumba,         kila kiumbe amekiumba.     W:  /:Yeye ni Baba Mwana           na Roho.:/ 2.  K:  Nguvu za Mungu          ni za ajabu,         Jinsi zilivyo hamna kifani.     W:  /:Yeye ni Baba ...:/ 3.  K:  Mle katika mikono yake         Yote hutunza          kwa usalama.     W:   /:Yeye ni Baba ...:/ 4.  K:  Yeye akaja kuishi kwetu,          Awe Mwokozi           wa wenye dhambi.     W:   /:Yeye ni Baba ...:/ 5.  K:  Roho katumwa kutufariji,          atuepushe           kwenye maovu.      W:   /:Yeye ni Baba ...:/ 6.  K:  Mungu M...

412. Mungu Ulisema

1. Mungu ulisema, giza ilikoma;     Twashukuru.    Twakusihi sote, duniani mwote,    na kwa watu wote, iwe nuru. 2. Yesu ulikuja, ulituletea     nuru kuu;    Macho kwa vipofu,     maisha kwa wafu:    nasi twakusifu, twashukuru. 3. Roho kiongozi, Roho wa mapenzi    tia nuru;    mwovu hata sasa     watu huwatosa.    Twakuomba hasa, iwe nuru. 4. Mungu wa Utatu,     mwanga wao watu,    tuwe nuru;    twende kwote, kwote,     wafundishwe wote:     duniani mwote iwe nuru.

413. Mungu yu Upande Wetu

1. Mungu Yu upande wetu    Anayetupigania.    Mungu Yu upande wetu    hakutuacha yatima.         :/:Roho Mtakatifu uje          utupe nguvu mpya          usituache         Mungu Yu upande wetu         hakutuacha yatima.:/:   2. Bwana ametujalia     baraka zake rohoni    twawezeshwa kwenda mbele,     kutimiza amri yake        :/:Roho Mtakatifu…  3. Ulitume neno lako,    utuwezeshe kunena;     tutimize amri yako     pembe zote za dunia.           :/:Roho Mtakatifu…  4. Mtakatifu, Roho Mwema     Tutumie kama chombo,     Utimize kazi yako,    Tukitii sauti yako.          :/: Roho Mtakatifu …

414. Mwokozi Umeokoa

1.  Mwokozi umeokoa      nimekuwa wako Wewe.      Damu imenisafisha,      Sifa kwa Mwana Kondoo.          Utukufu, Haleluya,          Sifa kwa Mwana Kondoo.           Damu imenisafisha,           utukufu kwa Yesu. 2.  Nilijitahidi sana      ila sikupata raha     bali kwa kumtegemea      nilipata baraka.            Utukufu Haleluya… 3.  Daima namwegemea     damu ikifanya kazi      Nikioga kwa chemchemi     itokayo Mwokozi.             Utukufu Haleluya… 4.  Sasa nimewekwa wakfu     nitaishi kwako Wewe:      Fahari nashuhudia      Ya wokovu wa bure.             Utukufu Haleluya... 5.  Nasimama kwake Ye...

415. Nasikia Kuitwa

1.  Nasikia kuitwa na sauti yako      Nikasafiwe kwa damu     Ya kwangikwa kwako.           Nimesongea Mtini pako,           unisafi kwa damu           ya kwangikwa kwako.  2.  Ni mnyonge kweli,      umenipa nguvu,     ulivyonisafi taka, ni utimilifu.            Nimesongea Mtini... 3.  Yesu hunijuvya; mapenzi,      imani, tumaini na amani      hapa na mbinguni.           Nimesongea Mtini... 4.  Huipa imara, kazi yake, ndani:      huongezeka neema,      ashindwe Shetani.            Nimesongea Mtini... 5.  Huishuhudia mioyo ya imani     ya kuzipata ahadi,      wakimuamini.            Nimesongea Mtini... 6.  Napata w...

416. Ndiyo Damu ya Baraka

1.  Ndiyo damu ya baraka      ituoshayo wakosa,     kwake Bwana twaokoka,     nasi twamsifu sasa.      Nimestahili hukumu,     siwezi kujitakasa     Nioshe katika damu,     Takuwa safi kabisa.     Safi kabisa; safi kabisa!      Nioshe katika damu      Takuwa safi kabisa. 2.  Yesu alivikwa miiba     Na kuangikwa Mtini,     Na maumivu si haba      Yaliyompata chini      Nataka kijito hicho      Niende kuoga sasa;      Ndicho kinitakasacho      Nami ni safi kabisa.     Safi kabisa, safi kabisa!      Ndicho kinitakasacho,      Nami ni safi kabisa. 3.  Baba, kweli nimekosa,      moyo wangu ni dhaifu;      Dhambi ni nyingi kabisa      Nipate wapi wokovu?      Yesu kiji...

417. Neno Lake Mungu Lakuita Wewe

K:  /:Neno  W:  Neno lake Mungu lakuita wewe,     Neno la wokovu, tena jema:/  1. K:  Yesu alisema:      W:  Mkahubiri;     K:  Neno lake Mungu,      W:  la wokovu.     K:  Neno... 2. K:  Enendeni kote,     W:  duniani;     K:  Pia mbatize,    W:  kwa Utatu.      K:  Neno...  3. K:  Wote tusimame,      W:  tusimame;     K:  tusikie Neno,     W:  la wokovu.      K:  Neno...  

418. Nimekombolewa na Yesu

1. Nimekombolewa na Yesu    Aliyenirehemia;    Kwa bei ya mauti yake    Nimekuwa mtoto wake            Kombolewa!             Nakombolewa na damu;            Kombolewa!            Mimi mwana wake kweli 2. Kukombolewa nafurahi,     Kupita lugha kutamka;    Kulionyesha pendo lake,    Nimekuwa mtoto wake.             Kombolewa! … 3. Nitamwona uzuri wake,    Mfalme wangu wa ajabu;     Na sasa najifurahisha katika    neema yake              Kombolewa! … 4. Najua taji imewekwa     Mbinguni tayari kwangu;     Muda kitambo atakuja    Ili alipo, niwepo              Kombolewa! …