371. Kwa Furaha ya Mbinguni

1. Kwa furaha ya mbinguni

   umeitwa roho yangu, furahi!

   Yesu akufungulia mlango wake,

   ruka kwake kama tai. 


2. Nitakaza mwendo sana

   nifikie kundi la wateule,

   waimbao na kusifu Bwana 

   Yesu pamoja na malaika.

 

3. Yesu Bwana wangu ng’oa 

   nanga ya mashua yangu upesi,

   niingie bandarini mwa amani

   na kuona raha kuu.


4. Yesu wangu sitakoma kukusifu,

   kwani umeniponya.

   Roho yangu yatamani kukuona;

   Bwana njoo, nichukue!


5. Unaweza kwa haraka 

   kugeuza woga uwe furaha.

   Unatupitisha kufa kama ndoto:

   mara tutafufuka.


6. Umevumilia shida hata kufa

   tusishindwe na kifo. 

   Sasa kufa kumeshindwa,

   nao mwili wangu utafufuka.

Popular posts from this blog

420. Ni Salama Mikononi Mwake

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

406. Mfurahini, Haleluya