420. Ni Salama Mikononi Mwake

1.  Ni salama mikononi mwake 

    Yesu Mwokozi akiwa  nami, 

    Nakingiwa na hatari zote

    Katika mkono wake. 

        :/katika (kiganja cha)  

          Mkono wake/: 

          Wala sina hofu siku zote, 

          Katika mkono wake.


2.  Hunishika mikononi mwake,

    Nina amani pendoni mwake 

    Mungu anitoa shaka zote

    katika mkono wake  

          :/katika (kiganja cha)

           Mkono wake/:...


3.  Anilinda wala haniachi 

    pendo lake wala halifichi,

    Atanipa nguvu siku zote 

    katika mkono wake  

           :/katika (kiganja cha)  

             Mkono wake/:...

Popular posts from this blog

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

406. Mfurahini, Haleluya