398. Hapana Rafiki Kama Yesu
1. Hapana rafiki kama Yesu,
Yu pekee, Yu pekee;
Hapana mpozi kama Yesu
Yu pekee, Yu pekee.
Yesu ajua shida zetu,
Aweza kutuongoza;
Hapana rafiki kama Yesu,
Yu pekee Yu pekee.
2. Yeye anaye sifa, ni Yesu
Yu pekee, Yu pekee;
Ndiye aliye Mnyenyekevu
Yu pekee, Yu pekee;
Yesu ajua......
3. Yesu pamoja nasi daima,
Yu pekee, Yu pekee;
Kwa usiku aleta salama,
Yu pekee, Yu pekee;
Yesu ajua......
4. Kulinda Yesu Yu Mwaminifu,
Yu pekee, Yu pekee;
Atawakubali wahalifu,
Yu pekee, Yu pekee;
Yesu ajua......
5. Alipelekwa awe Mwokozi,
Yu pekee, Yu pekee;
Anatutayarishia enzi
Yu pekee, Yu pekee;
Yesu ajua......