365. Sijui Njia Wewe Waijua

1.  Sijui njia, Wewe waijua,

    kwa hiyo moyo unatulia.

    Ni bure hata nikihangaika, 

    mchana kutwa hata na usiku.


2.  Wewe wajua njia hata mchana,

    umekwisha tengeneza vyote.

    Nakushukuru kwa upendo wako,

    wanipenda kwa huruma yako.


3. Upendo ukivuma waujua, 

   wautuliza tu huchelewi.

   Hunidanganyi na mimi nangoja,

   Wewe wajua njia, yatosha!


Popular posts from this blog

420. Ni Salama Mikononi Mwake

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

406. Mfurahini, Haleluya