410. Mtolee Bwana
1. Mtolee Bwana katika maisha
matunda ya pendo,
yale yapasayo,
tumtolee Bwana.
Tushukuru yale yatokayo kwake
kwa neema kubwa.
/:Tutoe sadaka
tumshukuru Bwana:/
2. Atupa maisha, akili, uweza;
atupa nyakati za kufanya kazi;
na hiyo ni neema.
Na mali nyingine zinatoka
kwake kutufurahisha.
/:Tusifu na nini
kwa vipaji vingi?:/
3. Sisi twazaliwa, katika ukiwa.
Mungu peke yake,
ndiye atoaye;
kwetu kwa huruma.
Tu wakili wake;
hayo tuyatunze na tusitawanye.
/:Kutoa tutoe;
talanta ni zake.:/
4. Fundisho ni kubwa:
Mjane katoa mali yake yote,
ya nyumbani mwake;
kumshukuru Bwana.
Kutoa ni haja;
tena ni ibada kwake Yesu Bwana.
/:Tutoe sadaka;
tumshukuru Mola.:/
5. Tunapochunguza tunavyotumia,
tutoe mioyo, tuache uchoyo;
kwani atupenda.
Kwa kila wakati;
yeye ni mlinzi, anatuongoza.
/:Tutoe kwa Bwana;
hili linapasa.:/
6. Ingawa Mwokozi Yeye ni tajiri
aliacha Yeye utajiri wake
kututajirisha.
Alibeba Yeye ufukara wote
kweli ni neema.
/:Kwa pendo katenda
kwetu yote mema.:/