346. Wajua Kuzihesabu Nyota

1.  Wajua kuzihesabu

    nyota zilizoko juu?

    Wajua kuyahesabu 

    nayo mawingu yote? 

    Mungu aliyahesabu 

    lisimpotee hata moja;

    avijua kwa majina

  

2.  Wajua kuwahesabu 

    na ndege wa angani? 

    Wajua kuwahesabu 

    samaki wa majini? 

    viumbe vyake vyote. 

    Mungu huwapa kuwapo

    huwaita kwa majina. 

    Kwa hiyo wanamchezea 

    na kumfurahia mno.


3.  Wajua kuwahesabu 

    watoto waamkao

    asubuhi vitandani, 

    wacheze mchana kutwa,

    Mungu huwatunza wote

    kwa huruma zake kuu; 

    wewe nawe akupenda,

    ndiye mpenda watoto.

Popular posts from this blog

420. Ni Salama Mikononi Mwake

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

406. Mfurahini, Haleluya