370. Baada ya Kazi na Taabu Zote
1. Baada ya kazi na taabu zote
nikiingia kwenye furaha,
kumwona Yesu,
kumwabudia,
kutakuwa furaha yangu kuu.
/: Kumwona tu ni furaha.:/
Nikiondolewa shida zote,
nikiona uso wa Bwanangu.
2. Mwenye rehema anipendaye
akinipa kikao mbinguni,
nitamfurahia Mponya wangu
kwa kumwona tu uso kwa uso.
Kumwona tu …
3. Pale mbinguni kwenye furaha
nitaonana na ndugu wengi.
Lakini kumwona Bwana Yesu
kutakuwa furaha kabisa.
Kumwona tu …