390. Bwana Asema Nimtume Nani
1. Bwana asema
Nimtume nani
/:Na ni nani
atakayekwenda
badala yetu:/
Nitume mimi Bwana
X 4 X 2
2. Midomo yangu
Michafu sana
/:Uichome kwa kaa
la moto unitakase:/
Nitume mimi....
3. Ninaogopa
Umri mdogo
/:Kuhubiri Neno lako
Bwana huko niendako:/
Nitume mimi....
4. Waniambia:
“Usiogope,
/:utapata ujasiri
mwingi: kutoka kwangu.”:/
Nitume mimi....