408. Mimi ni Mzabibu
W: Mimi ni mzabibu,
Mimi ni mzabibu,
nanyi ni matawi Yangu,
nanyi ni matawi Yangu.
1. K: Kaeni ndani yangu,
nami ndani yenu,
kwani mu matawi,
nami kweli ni mzabibu.
W: Mimi ni mzabibu,...
2. K: Nje yangu mimi,
hamwezi kuzaa,
kwani mu matawi,...
3. K: Tawi lizaalo, lizidi kuzaa,
kwani mu matawi, ....
4. K: Furaha yangu,
iwe ndani yenu,
kwani mu matawi,...
5. K: Ombeni lo lote
nanyi mtapewa,
kwani mu matawi,...
6. K: Amri yangu ndiyo,
mpate kupendana,
kwani mu matawi,...
7. K: Niliwachagua,
muwe rafiki zangu,
kwani mu matawi,...
8. K: Zaeni matunda,
yapate kukaa,
kwani mu matawi,...