391. Bwana Mungu, Nashangaa

1. Bwana Mungu,

   nashangaa  kabisa

   nikitazama kama vilivyo; 

   nyota, ngurumo, 

   vitu vingi vyote 

   viumbwavyo 

   kwa uwezo wako 

        /: Roho yangu na ikuimbie 

        Jinsi wewe ulivyo Mkuu.:/


2. Nikitembea pote duniani, 

   ndege huimba, nawasikia;

   milima hupendeza macho sana,

   upepo nao nafurahia 

       /:Roho yangu…


3. Nikikumbuka kama 

   Wewe Mungu 

   ulivyompeleka mwanao,

   afe, azichukue dhambi zetu

   kuyatambua ni vigumu mno. 

         /: Roho yangu.....


4. Yesu Mwokozi utakaporudi 

   kunichukua kwenda

   mbinguni, nitashukuru 

   na kwimba milele 

   Wote wajue jinsi ulivyo. 

        /:Roho yangu …


Popular posts from this blog

420. Ni Salama Mikononi Mwake

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

406. Mfurahini, Haleluya