378. Pana Jito, Lina Maji Mazuri

1.  Pana jito, lina maji mazuri,

    yaenda ulimwenguni. 

    Lametameta nalo linang’aa. 

    Walijua jito hilo?

    Ninakuita nawe njoo! 

    Utafute jito hilo! 

    Maji yake yapoza moyo. 

    Nawe yateke unywe.


2. Wanywao maji haya wafurahi,

   waimba kwa shangwe kubwa. 

   Makosa na shida yanaondoshwa,

   wote waoshwa na Bwana.

        Ninakuita nawe njoo …


3. Jito hilo latoa maji mengi, 

   matamu yapendezayo. 

   Yaponya wagonjwa, 

   yatia nguvu, uchafu watakasika. 

         Ninakuita nawe njoo…


4. Maji ya jito hilo ni uzima 

   unaotoka kwa Yesu. 

   Damu yake yenye kiasi kikuu 

   imemwagwa tusafike.  

        Ninakuita nawe njoo … 

Popular posts from this blog

420. Ni Salama Mikononi Mwake

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

406. Mfurahini, Haleluya