377. Atashuka na Mawingu
1. Atashuka na mawingu
aliyewambwa mtini,
na watakatifu wengi
watamtukuza sana.
/: Haleluya, Haleluya,
Haleluya, :/
Yesu anatujia!
2. Kila jicho litamwona
katika enzi yake,
nao waliombeza
wataogopa wote,
/: Watalia, watalia,
watalia, :/
wakimwona Mwokozi.
3. Na alama za vidonda
hata sasa anazo,
nao watumishi wake
wakombolewa nazo,
/: alipata, alipata,
alipata, :/
makovu kweli kwao.
4. Wapaangukia wote
penye kiti cha enzi.
Vaa Mwokozi nguvu zote
Njoo sasa kumiliki!
/: Njoo upesi! Njoo upesi!
Njoo upesi! :/
Tunakuomba Bwana.