381. Kuna Nchi Nzuri Sana
1. Kuna nchi nzuri sana
na utukufu mkubwa mno,
Neno hilo lapendeza,
siku nitakapofika!
2. Njia zake za dhahabu
na lulu za thamani kuu,
kuna na mengi ajabu,
siku nitakapofika!
3. Watu wake ni wazuri,
kwao hakuna wadhambi,
huishi kwa furaha tu,
siku nitakapofika!
4. Sauti zao ni nzuri,
huku hazipatikani,
ni sauti za ajabu,
siku nitakapofika!
5. Ndio watoto wa Mungu
wenye upendo wa kweli,
mavazi yao meupe,
siku nitakapofika!
6. Bwana wetu tuandae,
tuweze kufika huko,
ili tushiriki nao,
pawe ni makao yetu!