387. Anza Yote na Bwana
1. Anza yote na Bwana;
Umwamini kama mtoto
Anavyomwamini baba;
Nawe ufanye hivyo.
:/:Anza yote na
Bwana.:/:
2. Anza yote na Bwana;
Enyi wateule wake
Msipoteze lengo lake,
Nenda njia ya Bwana.
:/:Anza yote…
3. Anza yote na Bwana;
Uwe jasiri kwa Bwana,
akupa msaada wake,
Ufanye kazi yake
:/: Anza yote…
4. Anza yote na Bwana;
Atatuma roho wake
awe mfariji wako
Kwenye maisha yako
:/:Anza yote ....