400. Imezuka Siku ya Neema

1. Imezuka siku ya neema, 

   mfano wa pambazuko; 

   yenye mwanga toka 

   Mungu juu furaha ikamilishwe.

   Mungu ndiye nuru gizani

   akae mioyoni mwetu


2. Imezuka siku ya neema,

   Mwokozi katutokea; 

   ulimwengu wote upewe 

   furaha pasipo mwisho. 

   Yesu atupenda kabisa,

   fedheha amefukuza.


3. Alibeba dhambi, si zake,

   alipotundikwa mtini.

   Kifo hakikumweza Kristo. 

   Mwamba akauondoa,

   Ili sisi na jeshi la juu 

   tumwimbie siku zote.


4. Baada ya siku hamsini 

   akatumwagia roho,

   ili tusibaki gizani,

   na kupotelea mbali. 

   Moto wake watutakasa, 

   na kutuponyesha kweli. 


5. Safari ya mwisho yaiva, 

   tuitwapo naye Kristo. 

   Sote tutaimba kwa shangwe

   pamoja na wambinguni. 

   Tukiishi mwangani mwake,

   tukimhimidi milele.


Popular posts from this blog

420. Ni Salama Mikononi Mwake

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

406. Mfurahini, Haleluya