341. Haya, Umati wa Yesu

1. Haya, umati wa Yesu, 

   ulioungwa naye! 

   Haya, enendeni hima 

   katika vita kubwa! 

   Shetani tayari, 

   kupigana na sisi!


2. Tumfuate Yesu Kristo, 

   tumwamini Yeye tu. 

   Mwovu akituvizia 

   sisi hatuogopi.

   Majeshi ya mbingu

   ni pamoja na sisi!


3. Tukikesha na kuomba

   Yesu anavyotaka, 

   tukishika Neno lake

   na tukimtegemea 

   kwa nguvu hizi tu

   tutaweza kushinda!


4. Sasa haya wenzi wangu,

   tumfuate Yesu tu! 

   Siku za maisha yetu,

   tuwe katika yeye. 

   Tuache dunia

   kuingia mbinguni!


5. Pale Mungu atawapa 

   taji walioshinda, 

   wapate urithi wao 

   nyumbani mwa milele. 

   Hayani! Tuimbe,

   tumsifu Bwana wetu! 

Popular posts from this blog

420. Ni Salama Mikononi Mwake

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

406. Mfurahini, Haleluya