380. Mungu Tangu Mwanzo

1.  Mungu tangu mwanzo

    ameandaa

    wokovu kwa wote, pia na njia

    kwa wanaoishi, kutopotea.

    Waje kwake tena, awaridhia.

    Kayatimiza yote, 

    ya kuokoa wote 

    nitajiteteaje? Sina udhuru, 

    sina udhuru, 

    sina mbele za Mungu


2. Adamu wa kale, hakutubia,

   uasi kwa Mungu, ajitetea. 

   Hoja yake kubwa, kasingizia,

   Mungu kaamua, kuhurumia.

   Kayatimiza yote …


3. Maarifa mengi yameingia,

   na watu wazidi kwa kukosea 

   wavunja adili na uraia,

   Mungu sasa aja na mausia. 

   Kayatimiza yote …


4.  Maajabu mengi ya kuvutia,

    na wajumbe tele atutumia,

    alimtuma Yesu kutukomboa,

    akafanya mengi, na kutufia.

    Kayatimiza yote ...


5.  Sisi tukiishi atungojea, 

    atuvumilia, geuza nia. 

    Yaliyotupinga ameondoa,

    sasa deni letu, kuitikia.

    Kayatimizia yote …


6.  Kweli, ndugu yangu, 

    huna udhuru,

    Bwana wa hukumu, akituzuru,

    amefanya yote, tuwekwe huru,

    kwa hiyo tutubu na  kushukuru.

    Kayatimiza yote … 

Popular posts from this blog

420. Ni Salama Mikononi Mwake

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

406. Mfurahini, Haleluya