350. Maji Yako ya Akiba
1. Maji yako ya akiba
yatakapopungua
uwakarimu wenzako
wasafiri njiani,
na hayo yatawatosha,
safari yenu yote.
2. Kapu utakalotoa,
litajalizwa tena.
Vyakula vikipungua,
anga yafunguliwa
kilichotosha kwa mmoja,
kitatosha wawili.
3. Sadaka iliyo hai,
Mungu huibariki.
Ghala za dunia hii,
nondo watamaliza.
Utabarikiwa sana
hazina ya mbinguni.
4. Limbikiza juu mbinguni
kutu isikofika,
sadaka yako iliko
ndiko na moyo wako
utakapokaa nayo,
mbinguni juu milele.
5. Roho ipendayo ndugu
ni maji ya uhai
ukimtazama Mwokozi,
u tajiri mbinguni,
unapopenda wenzako,
huo ni uhai mpya.