389. Ashukuriwe Mwenyezi
1. Ashukuriwe mwenyezi.
Ametujalia mengi.
Ni ukarimu wake mkuu
kwetu milele.
Tuwe naye pote pote
duniani,
Tuwe naye pote,
(Tumsifu pote)
Safari hii yetu duniani.
Tukiwa naye mwenyezi
hatuna woga.
2. Hata tukiwa gizani,
mwanga wake watutosha.
kwa neno lake tapita
vipingamizi.
Tuwe naye pote pote....
3. Nazo hatari za njia,
zikitujia, ee Bwana,
msaada wetu ni wewe,
utawalaye.
Tuwe naye pote pote....
4. Tunatazama mbinguni,
utupe baraka yako.
Hatuna nguvu wenyewe,
utuendeshe.
Tuwe naye pote pote....