385. Nitayainua Macho Yangu

Nitayainua macho yangu 

niitazame milima. 

Msaada wangu utatoka wapi? 

Msaada wangu u katika Bwana. 

Aliyezifanya mbingu na nchi.

Asiuache mguu wako usogezwe. 

Asisinzie akulindaye. 

Naam, naam, naam. 

Hatasinzia wala hatalala usingizi. 

Yeye aliye mlinzi wa Israeli. 

Bwana ndiye mlinzi wako. 

Bwana ni uvuli

mkono wako wa kuume.

Jua halitakupiga mchana

wala mwezi wakati wa usiku. 

Bwana atakulinda 

na mabaya yote. 

Bwana atakulinda 

na mabaya yote. 

Atakulinda nafsi yako. 

Bwana atakulinda, 

Utokapo na uingiapo. 

Tangu sasa na hata milele 


 


Popular posts from this blog

420. Ni Salama Mikononi Mwake

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

406. Mfurahini, Haleluya