343. Mwana wa Mungu Atoka
1. Mwana wa Mungu atoka
kwenenda vitani,
bendera yake nyekundu;
utamfuata wee;
wataka kuungana
na maumivu yake?
Jitwishe msalaba wako,
nenda nyuma yake.
2. Stefano aliuawa
kwa kumtegemea
ndiye aliyemtazama
ashindaye kufa.
Yeye kama Bwana wake
wakati wa kufa,
akawaombea wale
waliomwumiza.
3. Na wale mitume tena
kumi na wawili,
Roho kawasaidia
kwenenda vitani.
Hawakuogopa kamwe
simba wala panga:
Roho utusaidie,
tukiwafuata.
4. Jeshi kubwa lasimama
waume na wake
mbele ya kiti cha Bwana
na nguo nyeupe.
Wakajiponya mbinguni
kushinda mashaka.
Ee Bwana, utubariki,
tukiwafuata!