359. Nikiwa na Yesu
1. Nikiwa na Yesu, akiwa nami:
Mpaka nitakapokufa
sisahau pendo lake,
sioni huzuni
naona furaha na amani.
2. Nikiwa na Yesu naacha vyote,
namfuata Bwana wangu
siku zote kwa bidii; sitazifuata
njia pana za dunia hii.
3. Nikiwa na Yesu nayatumia
mambo yote ya dunia
Baba anavyopenda
nikimjua Yeye
siogopi mambo ya dunia.
4. Nilipo na Yesu ndipo pazuri.
Ninapata mema yote
kama mrithi wa Mungu;
ninapewa ndugu wapya ndio
Wakristo wenzangu.