344. Watoto Wake Mungu
1. Watoto wake Mungu
imbeni safarini,
Mwokozi tutamsifu,
aliye mtakatifu.
2. Sote tu safarini,
tunakwenda mbinguni,
na tuone magumu,
jueni hayatakaa.
3. Watoto mwimbieni
inueni na macho!
Waliovumilia
wamekwisha ingia.
4. Ndugu tusiogope,
tutafika mbinguni,
Yesu akiwa nasi,
Shetani hatuwezi!
5. Bwana twakufuata,
ya chini twayaacha
U kiongozi wetu,
utatufikisha juu!