351. Nataka Nimjue Yesu

1.  Nataka nimjue Yesu,

    na nizidi kumfahamu, 

    nijue pendo lake, na 

    wokovu wake kamili. 

         Zaidi, zaidi,  

         nimfahamu Yesu, 

         nijue pendo lake, na 

         wokovu wake kamili.


2.  Nataka nimwone Yesu, 

    na nizidi kumsikia 

    anenapo Kitabuni, 

    kujidhihirisha kwangu.

         Zaidi, zaidi …


3.  Nataka nifahamu, na  

    nizidi kupambanua 

    mapenzi yake, nifanye 

    yale yanayompendeza.  

          Zaidi, zaidi …


4.  Nataka nikae naye,

    kwa mazungumzo zaidi,

    nizidi kuwaonyesha 

    wengine wokovu wake. 

          Zaidi, zaidi … 

Popular posts from this blog

420. Ni Salama Mikononi Mwake

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

406. Mfurahini, Haleluya