367. Mwokozi Yesu, Utangulie

1.  Mwokozi Yesu, utangulie 

    njia zote za maisha, 

    nasi tutakufuata, 

    utuongoze

    mpaka mbinguni!


2.  Tunapoona shida zozote, 

    tuzivumilie vema, 

    tukumbuke; yatupasa 

    kwenda mbinguni

    kwa shida nyingi.


3.  Mambo mabaya yakitujia,

    tukiona ndugu zetu 

    wanashikwa na huzuni, 

    utukumbushe:

    Raha i kwako!


4. Utuongoze njiani Yesu;

   utulize mioyo yetu 

   hata siku za huzuni. 

   Tufungulie

    mlango wa mbingu!


Popular posts from this blog

420. Ni Salama Mikononi Mwake

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

406. Mfurahini, Haleluya