358. Anayemtumaini Mungu
1. Anayemtumaini Mungu
siku zote kwa moyo mkuu,
ataona mastaajabu,
zikija shida na msiba.
Anayemngojea Mungu
amejenga juu ya mwamba.
2. Tukisumbuka mchana kutwa
sababu ya shida zetu:
Tukilia usiku kucha
sababu ya msiba wetu
ni bure: Twazidisha tu
uchungu wa msiba wetu.
3. Lakini tukivumilia
mizigo tuliyotwikwa,
na Baba yetu ajuaye
vizuri yanayotufaa,
tutapewa nguvu nyingi
za kuchukua huzuni.
4. Ameiweka saa tayari
ya kupunguza mizigo.
Tukiwa wenye welekevu
katika kuvumilia,
mara atatuokoa
na kututendea mema.
5. Katika shida usidhani:
“Mungu kaniacha sasa:
Lakini matajiri wote
anawapenda vizuri.”
Anageuza upesi
hali ya watu wowote.
6. Si kazi ngumu kwake Mungu
kukuza watu maskini,
kuwapunguza matajiri
wajikuzao wenyewe,
Mungu aweza upesi
kukuza na kupunguza.
7. Fuata njia yake Mungu
ufanye kazi kwa bidii,
umtumaini Mwenye enzi
Yeye atakubariki.
Amtegemeaye Mungu
hatakosa msaada wake.