409. Mjini Kwake Nazareti
1. Mjini kwake Nazaret
kasema Yesu wazi,
yakuwa kwake unabii
wa kale umetimia.
/:Kusaidia maskini,
vipofu nao waone,
wafungwa wawe huru tu,
wasetwa wawe wazima.:/
2. Wazee walishangazwa tu
na mahubiri yake.
Huenda huyu ni nabii
na hata Kristo Masihi.
/:Kusaidia maskini,...
3. Maisha’ke shuhuda kuu,
maneno yake kweli.
mpaka kufa kawa mtii,
kawambwa msalabani.
/:Kusaidia maskini,...
4. Wenzangu, muwe mashujaa,
kumshuhudia pote.
Mwokozi Yesu yu pekee,
na hivyo akatujia.
/:Kusaidia maskini,...