374. Nchi Nzuri Yametameta

1.  Nchi nzuri yametameta,

    huonekana kule mbali, 

    naye Yesu hutuongoza. 

    Tufike na sisi huko.

        /:Si mbali, karibu,  

        tutaimba na sisi huko!:/


2.  Kule tutawaona wengi

    wapendwao na Yesu Bwana,

    Tutashirikiana nao  

    itakuwa furaha kubwa.

          Si mbali …


3. Tutamwona na Bwana wetu,

   Yesu Kristo Mwokozi wetu,

   Tutashangilia daima, 

   tuna hamu ya kwenda kwetu. 

          Si mbali …


Popular posts from this blog

420. Ni Salama Mikononi Mwake

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

406. Mfurahini, Haleluya