372. Tegemea Mpaka Kufa

1. Tegemea mpaka kufa, 

   utapata wokovu.

   Bwana Yesu ni Mwokozi

   Yeye anakupenda.

   Uje kwake ’sikawie,

   Yeye akuokoa.

   Njoo upesi! Njoo upesi! 

   Fika kwa Bwana Yesu.


2. Acha mambo ya  dunia

   yakuhangaishayo.

   Iko mali ya uzima 

   unaitiwa hiyo.

   Mali hiyo ni uzima

   utapewa na Bwana. 

   Njoo upesi! …


3. Wakatae, waepuke 

   wanaokudanganya;

   ni wajinga, wakuponza, 

   wakupoteza wewe.

   Ila wewe ukatae 

   kuondoka kwa Yesu.

   Njoo upesi! …


4. Ukijua jambo hilo usipolifuata

   kosa hilo kubwa sana, 

   wapasiwa hukumu.

   Vumilia, jizuie utapata uzima.

        Njoo upesi! …


5. Bwana Yesu amekwisha 

   kukutengenezea 

   kitu chema kwake Mungu, 

   ndiko unakokwenda.

   Kile kitu upendacho 

   kule utakipewa.

        Njoo upesi! … 

Popular posts from this blog

420. Ni Salama Mikononi Mwake

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

406. Mfurahini, Haleluya