353. Twendeni Askari
1. Twendeni askari,
watu wa Mungu;
Yesu yuko mbele,
tumwandame juu;
Ametangulia Bwana vitani,
twende mbele
kwani ndiye amini.
Twendeni askari
watu wa Mungu:
Yesu yuko mbele,
tumwandame juu.
2. Jeshi la Shetani, likisikia
Jina la Mwokozi litakimbia
kelele za shangwe zivume nchi;
Ndugu inueni zenu sauti:
Twendeni …
3. Kweli kundi dogo,
watu wa Mungu,
sisi na mababa tu moja fungu,
hatutengwi nao, moja imani,
tumaini moja, na moja dini.
Twendeni...
4. Haya mbele watu nasi njiani.
Inueni mioyo nanyi sifuni;
Heshima na sifa ni ya Mfalme.
Juu hata chini, sana zivume.
Twendeni …