401. Jina la Yesu, Salamu!

1.  Jina la Yesu, salamu!

    Lisujudieni,

    ninyi mbinguni, hukumu

    na enzi mpeni.


2.  Enzi na apewe kwetu,

    watetea dini;

    mkuzeni Bwana Mungu wenu,

    na enzi mpeni.


3.  Enyi mbegu ya rehema, 

    nanyi msifuni;

    mmeponywa kwa neema,

    na enzi mpeni.


4.  Wenye dhambi kumbukeni

    Ya Msalabani,

    Kwa furaha msifuni,

    Na enzi mpeni


5.  Kila mtu duniani

    Msujudieni,

    Kote kote msifuni,

    Na enzi mpeni


6.  Sisi na wao pamoja 

    Tu mumo sifani, 

    Milele sifa ni moja, 

    Ni enzi mpeni. 

Popular posts from this blog

420. Ni Salama Mikononi Mwake

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

406. Mfurahini, Haleluya