368. Vumilia Utaona Mwisho
1. Vumilia utaona
mwisho kwamba umefika.
Kimebaki kitambo
kidogo tufike mbinguni.
/: Pokea (imani)
wokovu
ngao yako imani
nenda (mbele yake)
kwake Yesu Mwokozi:/
2. Kwa imani tutakwenda
mbele bila kulegea.
Wokovu ni wa thamani
kubwa kwa damu ya Yesu.
Pokea wokovu …
3. Wasikia sauti yasema
amini Injili,
ukiwa katika giza kubwa
amini Injili.
Pokea wokovu …
4. Imani kwa mambo
yaliyopo na yale yajayo,
mbele yetu ni njia ya kweli
Injili ya Yesu.
Pokea wokovu …