412. Mungu Ulisema

1. Mungu ulisema, giza ilikoma; 

   Twashukuru.

   Twakusihi sote, duniani mwote,

   na kwa watu wote, iwe nuru.


2. Yesu ulikuja, ulituletea 

   nuru kuu;

   Macho kwa vipofu, 

   maisha kwa wafu:

   nasi twakusifu, twashukuru.


3. Roho kiongozi, Roho wa mapenzi

   tia nuru;

   mwovu hata sasa 

   watu huwatosa.

   Twakuomba hasa, iwe nuru.


4. Mungu wa Utatu, 

   mwanga wao watu,

   tuwe nuru;

   twende kwote, kwote, 

   wafundishwe wote: 

   duniani mwote iwe nuru.

Popular posts from this blog

420. Ni Salama Mikononi Mwake

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

406. Mfurahini, Haleluya