345. Twalima na Kupanda
1. Twalima na kupanda
mbegu shambani tu,
kukuza, na kustawisha
ni nguvu ya Mungu.
Umande hata mvua
na jua na mwezi,
anayetupa haya
ni Baba Mwenyezi.
Vitu vyote vyema
vyatoka kwake tu,
kwa hiyo tumsifuni,
tumshukuru Mungu!
2. Vya mbali, vya karibu,
vyatoka kwa Mungu,
jua, mwezi na nyota,
kindege, bahari,
mimea ya mwituni,
vyakula vya shamba,
kwa mchana joto kali,
baridi usiku.
Vitu vyote …
3. Ndiye aongozaye
mzunguko wa jua,
ni chimbuko la mwezi,
mwendo wa dunia.
Huwalisha wanyama,
wapate chakula,
watoto wetu pia
wakae na afya.
Vitu vyote …