411. Mungu Mtatu Ndiye Muumba
1. K: Mungu Mtatu
ndiye Muumba,
kila kiumbe amekiumba.
W: /:Yeye ni Baba Mwana
na Roho.:/
2. K: Nguvu za Mungu
ni za ajabu,
Jinsi zilivyo hamna kifani.
W: /:Yeye ni Baba ...:/
3. K: Mle katika mikono yake
Yote hutunza
kwa usalama.
W: /:Yeye ni Baba ...:/
4. K: Yeye akaja kuishi kwetu,
Awe Mwokozi
wa wenye dhambi.
W: /:Yeye ni Baba ...:/
5. K: Roho katumwa kutufariji,
atuepushe
kwenye maovu.
W: /:Yeye ni Baba ...:/
6. K: Mungu Mtatu ana huruma
Njooni tumwendee,
tumwungamie.
W: /:Yeye ni Baba ...:/