347. Walio Watu Wake
1. Walio watu wake,
awajua Bwana.
Wakubwa na wadogo
nchini popote.
Awahifadhi vyema,
hawataangamia.
/: Waishipo, wafapo
ni wake daima. :/
2. Ajua kundi lake katika imani.
Wategemea yale wasiyoyaona.
Wazaliwa kwa Neno,
kwa Neno walelewa
/: nao kanuni yao
ni Neno la Mungu. :/
3. Ajua watu wake katika ushujaa
wa tumaini lao usio mashaka.
Ni miti istawiyo
katika mwanga wake,
/: mizizi yao hunywa
maji ya uzima. :/
4. Ajua watu wake katika upendo
uzaao tunda jema
lipendezalo mno.
Hupenda ndugu zao
alivyotupenda,
/: na wao hubariki
wabarikiwavyo. :/
5. Tusaidie, Bwana,
tupate imani, tumaini
lidumu, upendo uzidi.
Na siku zikifika
za kukuona Wewe.
/: tupate kusimama
kuumeni kwako. :/