405. Mbele Nina Endelea
1. Mbele ninaendelea,
ninazidi kutembea;
Maombi uyasikie,
Ee Bwana, unipandishe.
Ee, Bwana, uniinue,
kwa imani nisimame;
nipande milima yote,
Ee Bwana, unipandishe.
2. Sina tamani nikae,
mahali pa shaka, kamwe;
Hapo wengi wanakaa,
kuendelea naomba.
Ee, Bwana....
3. Nisifungwe na dunia,
asumbuapo Shetani;
natazamia mbinguni,
nitafika na imani.
Ee, Bwana....
4. Nataka nipandishwe juu,
zaidi yale mawingu;
nitaomba nifikishwe,
Ee, Bwana, unipandishe.
Ee, Bwana....