414. Mwokozi Umeokoa

1.  Mwokozi umeokoa 

    nimekuwa wako Wewe. 

    Damu imenisafisha, 

    Sifa kwa Mwana Kondoo.

         Utukufu, Haleluya,

         Sifa kwa Mwana Kondoo. 

         Damu imenisafisha, 

         utukufu kwa Yesu.


2.  Nilijitahidi sana 

    ila sikupata raha

    bali kwa kumtegemea 

    nilipata baraka. 

          Utukufu Haleluya…


3.  Daima namwegemea

    damu ikifanya kazi 

    Nikioga kwa chemchemi

    itokayo Mwokozi. 

           Utukufu Haleluya…


4.  Sasa nimewekwa wakfu

    nitaishi kwako Wewe: 

    Fahari nashuhudia 

    Ya wokovu wa bure. 

           Utukufu Haleluya...


5.  Nasimama kwake Yesu 

    ameponya roho yangu,

    Ameniondoa  dhambi 

    anifaye mzima. 

           Utukufu Haleluya…


6.  Nilifungwa kifungoni

    niliteswa nazo dhambi

    Nilifungwa minyororo 

    Yesu kanifungua  

          Utukufu Haleluya…


7.  Sifa ameninunua! 

    Sifa, nguvu za wokovu!

    Sifa Bwana huhifadhi! 

    Sifa zake milele  

          Utukufu Haleluya… 


Popular posts from this blog

420. Ni Salama Mikononi Mwake

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

406. Mfurahini, Haleluya