360. Ninamwambia Mungu

1.  Ninamwambia Mungu 

    aliye Mwenye enzi 

    mambo yangu yote. 

    Asiposaidia

    kwa tendo na baraka 

    siwezi kutenda kitu.


2.  Nikisumbuka sana, 

    usiku hata mchana,

    ni bure kabisa.

    Mungu  atamaliza 

    shughuli zangu zote 

    kama Yeye apendavyo.


3.  Namtumaini Bwana 

    anayenikingia

    hatari na shida. 

    Nikimfuata Yeye 

    sitaona hasara, 

    sitapungukiwa kitu.


4.  Ana huruma nyingi

    aondoa maovu, 

    afuta makosa. 

    Nijapokosa mengi,

    hatanitupa mimi,

    rehema yake ni kubwa.


5.  Nimempa Bwana huyu 

    moyo na mwili wangu,

    hata kufa kwangu.

    Akiniita kwake,

    nitafuata hima.

    Shauri lake ni jema tu.


6.  Moyo wangu, tulia!

    Umtumaini Bwana 

    aliyekuumba. 

    Kumbuka: Baba yako

    atakusaidia,

    hakosi shauri lolote.

Popular posts from this blog

420. Ni Salama Mikononi Mwake

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

406. Mfurahini, Haleluya