379. Kule Mbinguni Nataka Kwenda
1. K: Kule mbinguni nataka
kwenda, nitawezaje
kufika huko?
W: Yesu ni njia tena Uzima,
Tukimwamini
ndipo twafika.
2. K: Kule mbinguni
ni kwema sana,
Ndiko maskani
kwa Mungu Baba.
W: Yesu ni njia, tena Uzima,
Tukimwamini
ndipo twafika.
3. K: Mungu Mwenyezi
Mwenye uzima,
Ndiye mleta wetu uzima
W: Yesu ni njia, tena Uzima,
tukimwamini
Baba twamwona.
4. K: Mungu ni pendo,
apenda watu
Wafike kwake,
wawe wazima.
W: Yesu ni njia, tena Uzima,
Tukimwamini
Baba twamwona.
5. K: Tumwombe Baba
atupe Roho,
Kutuongoza tupate fika.
W: Yesu ni njia, tena Uzima,
Tukimwamini
Baba twamwona.
6. K: Kule mbinguni,
tukishafika,
Tutafurahi na kupendezwa.
W: Yesu ni njia, tena Uzima,
Tukimwamini
Baba twamwona.
7. K: Hapa tulipo uzima haba,
wenyeji wetu
kule kwa Baba.
W: Yesu ni njia, tena Uzima,
Tukimwamini
Baba twamwona.
8. K: Siku ya leo ni njema sana,
Na tumwandame,
Yesu ni njia
W: Yesu ni njia, tena Uzima,
Tukimwamini
Baba twamwona.