376. Yasikilizeni Haya
1. Yasikilizeni haya
watu wa dunia wote:
Mwokozi mara ya pili
yuaja atuamue.
2. Haji tena kama kwanza
na hali ya umaskini.
Ila kwa kuzionyesha
nguvu zake duniani.
3. Hao wampendao sasa
weupe hata weusi.
Watamwona akishuka
na enzi kuu mawinguni.
4. Siku hiyo ya hukumu
mimi nitakuwa wapi,
watakapoitwa wote,
walalao kaburini?
5. Yesu Bwana nakuomba:
Sasa unihurumie,
kuitenda kazi yako,
hata urudipo hapa!