361. Umngojee Bwana
1. Umngojee Bwana,
moyo wangu,
umwambie yote,
ana huruma.
Acha hofu, jua likicha
giza linashindwa
na mchana mzuri.
Huzuni zako zikizidi,
Mungu wa rehema
akulinda.
2. Umngojee Bwana,
moyo wangu,
umwambie yote,
ana huruma.
Zikivuma nguvu za
mwovu:
Bwana anaweza
kunyamazisha.
Wewe mwokozi,
nakungoja; niokoe nami,
Mungu wangu!
3. Umngojee Bwana,
moyo wangu,
umwambie yote,
ana huruma.
Masumbuko yote yaisha
na kilio chetu kitageuzwa,
tutaipata raha bora.
Tumshukuru Bwana
Mungu wetu.