382. Kuna Nchi Nzuri Isiyo na Dhambi
1. Kuna nchi nzuri isiyo na dhambi,
/: Wazee wema,
wazee wema
waimba haleluya. :/
2. Kuna nchi nzuri haina majonzi,
/: Wazazi wema
wazazi wema
waimba haleluya. :/
3. Kuna nchi nzuri isiyo na taabu,
/: Watoto wema,
watoto wema
waimba haleluya. :/
4. Kuna nchi nzuri isiyo na shida,
/: Vijana wema,
vijana wema
waimba haleluya. :/
5. Kuna nchi nzuri haina majuto,
/: Watoto wema,
watoto wema
waimba haleluya. :/
6. Na sisi twendeni
kwenye nchi hiyo.
/: Tuimbe pamoja,
tuimbe pamoja
Yesu Haleluya. :/