364. Mwanga Mkuu Ujao

1. Mwanga mkuu ujao, 

   utuangaze!

   Tuyapambanue vema

   maovu na mambo mema,

      /: Utuangaze. :/


2. Tulivyo duniani

   hatuna wema,

   macho yanaona woga,

   mioyo inatetemeka, 

     /: Hatuna wema. :/


3. Yesu tu ni Mwanga 

   wenye furaha.

   Tupe kuitumaini

   enzi ya utengemano,

      /: Yenye furaha. :/


4. Mwanga mkuu ujao,

   utuangaze! 

   Roho zetu ziinuke,

   na miguu ipate nguvu,

       /: Utuangaze! :/ 

Popular posts from this blog

420. Ni Salama Mikononi Mwake

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

406. Mfurahini, Haleluya