407. Mibaraka Tupe Mibaraka

1. Mibaraka tupe mibaraka

   Mibaraka tupe mibaraka 

   Toka kwako.

   Mungu Baba Mungu twakuomba,

       /:Tunakuomba libariki

   Kanisa lako Baba:/ 

   Liwe na umoja na upendo. 


2. Wachungaji na Maaskofu,

   Wachungaji na Maaskofu

   wabariki,

   Na Wainjilisti wabariki. 

   /:Uwape moyo wa hekima 

   katika kazi yako:/

   Wajenge Kanisa kwa upendo


3. Mungu Baba Mungu twakuomba

   Mungu Baba Mungu twakuomba

   tubariki;

   Hata na Wakristo wabariki 

  /:utupe moyo wa hekima katika

   kazi yako:/ 

   Tujenge Kanisa kwa upendo.


4. Waamini pote duniani Waamini

   pote duniani wabariki;

   Hata na Wazee wa Kanisa

   /:uwape moyo wa hekima 

   katika kazi yako:/

   Wajenge Kanisa kwa upendo.


Popular posts from this blog

420. Ni Salama Mikononi Mwake

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

406. Mfurahini, Haleluya