362. Umwekee Mwenyezi

1. Umwekee Mwenyezi 

   huzuni na shida

   ulizo nazo kwako,

   ana nguvu zote

   Bwana atulizaye 

   bahari na pepo, 

   aweza kutuliza

   hata moyo wako.


2. Bwana apenda sana

   kubariki watu, 

   wanaokuja kwake 

   wakimtumaini. 

   Ukisumbuka sana

   kwa uchungu mwingi,

   hupati kitu kwake:

   Ila ukimwomba.


3. Njia yako ikiwa 

   na giza na shida;

   anazo njia Yeye 

   za kukuokoa.

   Hakuna awezaye 

   kumzuia Mungu, 

   akitaka kufanya 

   mambo yake makuu.


4. Umtegemee Mungu 

   ukiona shida,

   ana rehema nyingi

   atakukumbuka,

   saa yake ikifika.

   Ungoje wakati

   wa Bwana, utaona 

   jua la furaha.


5.  Naye akikawia 

    kukusaidia,

    na giza likizidi,

    usione shaka: 

    Ataka kujaribu

    tegemeo lako. 

    Halafu aondoa 

    shida zako zote.


6. Atafanya vizuri 

   vyote uombavyo; 

   Umtegemee Mungu 

   na kumtumaini.

   Mwisho utaingia 

   mlangoni pa mbingu, 

   ndipo utamwimbia 

   nyimbo za kumsifu.


Popular posts from this blog

420. Ni Salama Mikononi Mwake

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

406. Mfurahini, Haleluya