375. Ni Wako Mungu, U Furaha Yangu
1. Ni wako Mungu,
u furaha yangu,
ni neema kumjua
Mwokozi wangu.
Haleluya atukuzwe,
Haleluya amen;
Haleluya atukuzwe,
ukarudi Yesu!
2. Mwana wa Mungu
ndiye fungu langu,
moyo wanitulia
kwa Yesu wangu.
Haleluya, atukuzwe, ...
3. Nikishapatwa
na mapenzi haya,
nimepata uzima
na mbingu pia.
Haleluya, atukuzwe, …
4. Nchi niendayo,
nenda mbio mbio
ina karamu kweli,
ya humu siyo,
Haleluya, atukuzwe, …
5. Twaionja humu
tulimo nchini,
mpaka tufike kwako
huko mbinguni.
Haleluya, atukuzwe, …