416. Ndiyo Damu ya Baraka

1.  Ndiyo damu ya baraka 

    ituoshayo wakosa,

    kwake Bwana twaokoka,

    nasi twamsifu sasa. 

    Nimestahili hukumu,

    siwezi kujitakasa

    Nioshe katika damu,

    Takuwa safi kabisa.

    Safi kabisa; safi kabisa! 

    Nioshe katika damu 

    Takuwa safi kabisa.


2.  Yesu alivikwa miiba

    Na kuangikwa Mtini,

    Na maumivu si haba 

    Yaliyompata chini 

    Nataka kijito hicho 

    Niende kuoga sasa; 

    Ndicho kinitakasacho 

    Nami ni safi kabisa.

    Safi kabisa, safi kabisa! 

    Ndicho kinitakasacho, 

    Nami ni safi kabisa.


3.  Baba, kweli nimekosa, 

    moyo wangu ni dhaifu; 

    Dhambi ni nyingi kabisa 

    Nipate wapi wokovu? 

    Yesu kijitoni pako

    naja naamini sasa 

    Nioshe kwa damu yako,

    Takuwa safi kabisa.

    Safi kabisa, safi kabisa! 

    Nioshe kwa damu yako, 

    Takuwa safi kabisa. 

 

Popular posts from this blog

420. Ni Salama Mikononi Mwake

398. Hapana Rafiki Kama Yesu

406. Mfurahini, Haleluya